JESHI LA POLISI MKOANI ARUSHA LATOA TAARIFA YA USALAMA KWA MWAKA 2016
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo.Picha na Vero Ignatus Blog
Pikipiki zilizokamatwa zikiwa zimepaki makuu ya polisi mkoa wa Arusha. Picha na Vero Ignatus Blog.
Magari yaliyokamatwa kwa makosa mbalimbali yakiwa yamepakiwa makao makuu ya polisi mkoani Arusha .Picha na Vero Ignatus Blog
Baadhi ya magari yaliyopata ajali yakiwa
Baadhi ya Magari yaliyopata ajali na kukamatwa kwa makosa yakiwa yamepaki katika kituo kikuu cha polisi mkoani Arusha .Picha na Vero Blog
Na.Vero Ignatus ,Arusha.
Jeshi la polisi mkoa wa Arusha limetoa taarifa juu ya
usalama barabarani kuanzia Januari 2016 –Desemba ,ambapo limesema kuwa takwimu
za kiahalifu zimepungua kwa makosa 383 ambapo mwaka 2015 kulikuwa na makosa
2,976 yaliyoripotiwa kwa kipindi cha kuanzia januari hadi desemba ,tofauti na
makosa yaliyoripotiwa 2016 ni 2,596.
Akitoa taarifa
hiyo kwa waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo
amesema kuwa mafanikio ya mapungufu ya makosa ya kiuhalifu 383 ni sawa na
asilimia 6.8%,na hii ni kutokana na juhudi za kila siku za jeshi la polisi
,vyombo vy a habari, pamoja na wananchi.
Amesema kuwa
makosa makubwa ya kuwania mali ikilinganishwa na mwaka 2015,wizi wa
silaha,ambapo yalikuwa makosa mawili,kipindi cha 2016 hakukuwa na tukio lolote
la namna hiyo,makosa ya udanganyifu kwa kutumia silaha 2015 yalikuwa 56,ambapo
mwaka 2016 yalikuwa 9 ni sawa na upungufu wa makosa 47.
Makosa ya
wizi wa pikipiki mwaka 2015 yalikuwa 247 mwaka 2016 makosa 59 pungufu ya makosa 188
ambapo makosa ya unyang’anyi wa kutumia nguvu 2015 yalikuwa 194 , mwaka 2016
yalikuwa makosa 70 hii pungufu ya makosa 124
Kamanda
amesema kuwa Makosa ya wizi wa magari nayo yalipungua ambapo mwaka 2015 yalikuwa
makosa 247 mwaka 2016 makosa 59 tofauti makosa 188,makosa ya wizi wa kuiba
kwenye mabenki mwaka 2015 yalikuwa 56 mwaka 2016 hakukuwa na kosa
lililoripotiwa,makosa ya uvunjaji wa nyumba
59 ambapo mwaka 2015 yalikuwa 900tofauti na mwaka 2016 yaikuwa makosa
841.
Makosa ya
kuwania mali ambayo yaliongezeka ni kughushi ambapo mwaka 2015 kulikuwa na
makosa 75 na mwaka 2016 yalikuwa makosa 93 sawa na ongezeko la makosa 6 ambapo
jumla yalikuwa 47,makosa makubwa ya jinai nayo kwa asilimia kubwa
yalippungua ambapo makosa 64 yalitokea
2016 ikiwa ni pungufu ya makosa 13 huku makosa ya kubaka kwa mwaka 2015 yakiwa 170
tofauti na mwaka 2016 yalikuwa makosa 142
pungufu ya makosa 28
Makosa ya kulawiti katika kipindi cha mwaka 2015
yalikuwa 48 ambapo 2016 makosa hayo
yalipungua ahadi kufikia 41 ikiwa ni
pungufu ya makosa 7,huku makosa ya kutupa
watoto yalipungua kwa makosa 9 ambapo 2016yalikuwa 25. wakati huohuo makosa ya wizi wa watoto kulikuwa na ongezeko la
makosa 2 ukilinganishwa na mwaka 2016
,ikilinganishwa na mwaka 2015 ambapo takwimu zinaonyesha kulikuwa na makosa 4 tofauti na mwaka 2016 kulikuwa na makosa 6.
Kamanda
aliendelea kusema kuwa katika kipindi cha mwaka 2016 ,makosa dhidi ya jamii yalipungua kutoka makosa 2,979 mwaka 2015
hadi kufikia makosa 2,596 mwaka 2016.makosa hayo yapo kama ifuatavyo:kupakia
silaha 2015 makosa 7,mwaka 2016 kosa lilikuwa 1,Nyara za serikali 2015 makosa
30 mwaka 2016 makosa 17,kupatikana na magendo 2015 makosa 4,tofauti na mwaka
2016 makosa 3.
Kamanda
Chalers Mkumbo amesema kuwa katika hatua nyingine hali ya usalama barabarani
mkoani Arusha 2016 ilizidi kuimarika tofauti na mwaka 2015,takwimu zinaonyesha
kuwa mwaka 2015 kulikuwa na jumla ya ajali 85 tofauti na mwaka 2016 kulikuwa na
ajali 70 ambapo upungufu ni ajali 15,Vifo vilikuwa 49 mwaka 2015 mwaka 2016
vilikuwa 44 pungufu kwa makosa 5 hukun takwimu zikionyesha watu waliokufa kwa
ajali hizo mwaka 2015walikuwa 54,tofauti na mwaka 2016 walikuwa 50.
No comments