GODBLESS LEMA AACHIWA HURU KWA DHAMANA ,ASEMA ANA WARAKA MAALUMU KWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema akishuka kutoka kwenye gari ya magereza tayari kwa kuyingia mahakamani.Picha na Vero Ignatus Blog

Waziri mkuu mstaafu mhe,Edward Ngoyai Lowasa akiwa nje ya mahakamabaada ya mahakama kutoa muda wa dk 15 kwa upande wa serikali kuombakuomba kuwasilisha hati zao za msingi na upande wa utetezi kusema wataijibu baada ya saa moja ambapo upande wa jahmuri walisema watatoa uamuzi saa saba na nusu
Mamia ya watu wakiwa nje wamuda kiwa wanasubiria muda ufike wamahakama itoe uamuzi
|
|
Wafuasi wa chdema wakimshangilia mbunge wa Arusha mjini anaonekana pichani baada ya dhamana kupatikana.Picha na Vero Ignatus Blog.
Baada ya Lema kupewa dhamana mambp yalikuwa hivi kama inavyooonekana pichani.Picha na Vero Ignatus Blog
| Baadhi ya wafuasi wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema)wakiwa wamevaa tisheti wakiwa na mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema baada ya kupewa dhamana.Picha na Vero Ignatus blog. |
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema akipokewa kwa furaha na mmoja wa
watoto wake alipowasili nyumbani kwake hii leo akitoka mahabusu.
Wanafamilia, ndugu jamaa na marafiki wakiwa na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alipowasili nyumbani kwake hii leo.
Hatimae Mahakama kuu kanda ya Arusha imemuachia kwa dhamana Mbunge wa
jimbo la Arusha mjini Godbles Lema baada ya kusota rumande kwa miezi minne
Mbunge huyo ameachiwa kwa dhamana ya sh milioni moja
pamoja na wadhamini wawili wenye vitambulisho vinavyotambulika na serikali
Akisoma
hukumu ya Mbunge Lema katika Mahakama Kuu Arusha Jaji aliyekuwa
akisikiliza kesi hiyo Salma Magimbi amesema kuwa Mbunge Lema hakupaswa
kukaa mahabusu kwa muda mrefu kwani ilipaswa kupewa dhamana.
Jaji magimbi amesema kuwa wanamwachia lema kwa dhamana hiyo
ya milioni moja ambapo kiasi hicho kimetolewa kwa njia ya bondi huku
wadhamini wawili nao wakiwa na vigezo vya dhamana.
Akizungumza
nje ya Mahakama hiyo Mbunge Lema amesema kuwa Jamhuri ilikuwa na nia ya
kumfunga lakini mungu amempigania mpaka kutoka
huku akimshukuru mke wake kwa jinsi alivyomfariji kwa kipindi akiwa
ndani.
Lema amesema kuwa Alisema kwa sasa ameandaa waraka wa kumwandikia raisi
kuwa wapo watu wanaoteseka bila kuwa na hatia magereza na kwamba atautoa siku za hivi karibuni
Nae wakili mtetezi wa Lema, Peter Kibatala amesema
kuwa Mahakama kuu imelekeza kuwa mahakama za chini zisimamie madaraka
yake na mamlaka yake bila kuyaachia na hivyo kwa sasa wanatakiwa
kujiandaa kwa ajili ya kupambana na kesi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe amesema kuwa
wanamkaribisha tena Lema Bungeni na kwamba kamati ya chama imemaliza
vikao vyake mjini hapa na kuwashukuru wabunge wa mikoa mbali mbali
waliofika kutetea dhamana ya lema.
Aidha Mbowe amelaani vikali kitendo cha jeshi la polisi
kutumia mamlaka yao vibaya kwa kuwapiga wananchi bila makosa kwa madai
kuwa wanakuja kuleta vurugu huku lengo ni kuja kusikiliza mbunge wao.



No comments