KITAIFA Watuhumiwa wa makosa ya ugaidi wamesema hawatahudhuria tena mahakamani
Na,Vero Ignatus,Arusha.
Watuhumiwa hao 61 wa makosa ya Ugaidi Arusha mapema leo asubuhi walimuhakikishia Hakimu Nestory Banda kuwa tarehe 11/04/2017, Hawatahudhuria tena mahakamani hapo hadi upeleezi utakapokamilika.
" Ni zaidi ya miaka minne sasa kila tukija mahakamani hapa mnatuambiwa kuwa upelelezi haujakamilika ,hata R.C.O alivyokuja kutuona mwezi wa kwanza mwaka huu alituahidi kuwa ndani ya miezi miwili upelelezi utakuwa umekamilika sasa tunashangaa mpaka sasa hivi hakuna lolote linaloendelea"
Hakimu anaendesha kesi hiyo Nestory Banda amewaambia watuhumiwa hao siku ya tarehe 11 ni lazima wahudhuria mahakamani .
"Nawaaahidi kwamba mara baada ya kumaliza shughuli za ki Mahakama kwa leo nitampigia simu R.C.O wala msiwe na taabu nyie njooni mahakamani "
Pichani ni baadhi ya watuhumiwa walivyowasili Mahakamani.
Gari iliyobeba mahabusu wa kesi ya ugaidi likiondoka Mahakamani kuelekea gereza kuu la Arusha
No comments