Ajali Mbaya ya Lori lililobeba mawe, Laua Mtu Mmoja

Makete

Lori lililokuwa limebeba mawe limepinduka katika kijiji cha Masisiwe na kusababisha majeruhi na kifo cha mtu mmoja ambaye alikuwa katika lori hilo


Taarifa za awali kutoka eneo la tukio zinasema kuwa lori hilo limepoteza muelekeo ghafla kisha likaanza kupinduka kwa kubiringika mara kadhaa umbali unaokadiriwa kuwa zaidi ya mita 80 kutoka barabarani

Ajali hiyo inadaiwa kutokea kati ya saa nane na saa tisa alasiri hii leo

Baadhi ya mashuhuda waliokuwa eneo la tukio ambao hawakutaka kutaja majina yao wamesema Lori hilo lilikuwa linatoka kubeba mawe kwa ajili ya kujenga daraja katika kata ya Ipepo ndipo lori hilo lilipopoteza mwelekeo likiwa njiani na kupinduka kisha kuporomokea bondeni

Jeshi la polisi Makete limefika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu kwa uchunguzi zaidi

Tutawaletea taarifa kamili ya tukio hilo pindi mamlaka husika zitakapatia

Polisi wakipima jinsi ajali hiyo ilivyotokea 
 Askari Polisi akiangalia mawe yaliyokuwa yamebebwa na lori hilo kabla ya kutokea ajali





Mwili wa marehemu ukiingizwa kwenye gari

Mwili wa marehemu ukiwa ndani ya gari la polisi
Lori hilo likionekana kwa mbali baada ya ajali


Muonekano wa lori hilo baada ya ajali





Ajali ilipoanzia, hapa ndipo lori hilo lilipotumbukia 

habari/picha na Edwin Moshi wa Eddy Blog

No comments