SIMBA YAIBUKA KIDEDEA DHIDI YA MADINI FC
Mashabiki wa timu zote mbili waliwa katika uwanja wa Shekhe Amri Abeid Uliopo jijini Arusha .Picha na Vero Ignatus Blog.Timu zote mbili Simba SC pamoja na Madini SC ,wakiwa wanaingia uwanjani tayari kwa mpambao,Picha na Vero Ignatus Blog

Baadhi ya mashabiki wa timu zote mbili wakisubiria mechoi iaza.Picha na Vero Ignatus Blog
Na.Vero Ignatus Arusha.
Club ya soka ta simba imefanikiwa kutinga hatua ya nusu
fainali ya kombe la shirikisho Tanzania baada ya kuilaza Madini ya
Arusha bao moja Kwa bila
Koncha msaidizi wa simba Jackson Mayanja amewashukuru
wapenzi wa Simba Kwa kujitokeza Kwa wingi kuliko vile ambavyo walikuwa
wanategemea.
Mayanja amesema kiwa changamoto kubwa waliyokumbana nayo
katika mchezo huo ni pamoja na hali ya uwanja in mbovu hauna nyasi za
kutosha jambo ambalo limepelekea Simba kukosa mabao mengi.
Aidha Goli hilo lililoipa simba ushindi lilifungwa kipindi cha pili na Loudit Mavungo (11)dakika ya 60.
Mayanja amesema kesho wanakwenda kucheza mchezo wa kirafiki
mererani ambapo hakutaja watachacheza mechi hiyo na timu ipi ambapo
wakimaliza jumanne wataanza safari kurudi Dar es salaam.
Kwa upande wake kocha wa timu tya Madini Fc Abdallah Juma
amesema kuwa timu yake ipo vizuri japo kuwa wamefungwa goli moja lakini
Vijana wameonyesha uwezo walionao na huu ni mwanzo mzuri kwao.
Aidha katika mtanange huo mchezaji wa timu ya simba
Ibrahimu Ajibu katika kipindi cha kwanza dakika ya 34 alipewa kadi ya
manjano.

No comments