Tanzania: Habari ya uongo ya Trump yawaponza wafanyakazi TBC
Shirika la utangazaji nchini
Tanzania TBC, limewasimamisha kazi wafanyakazi tisa baada ya taarifa za
uongo kuwa Rais wa Marekani Donald Trump, alimpongeza rais John
Magufuli, kupeperuswa hewani.
"Makosa hayo hayangefanyika ikiwa taratibu za uhariri zingefuatwa," Mkurugenzi mkuu wa TBC Ayub Chacha alisema.
Taarifa hiyo ya uongo inasema kuwa Trump alimtaja magufulia kama "shujaa wa Afrika", wakati akiweka sahihi sheria ya kuwazuia waafrika kutoka nchi ambazo marais hawafanyi lolote pamoja na wale wamekatalia madarakani.
Raia wa Tanzania hawatazuiwa kuingia Marakani, taarifa hizo zilisema
No comments