WAZIRI MAKAMBA ATOA MAAGIZO KWA MAMLAKA YA NGORONGORO
Na Lulu Mussa,Ngorongoro
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais mwenye dhamana ya usimamizi wa Mazingira nchini Mhe. January Makamba amesema kuwa ni lazima hatua za haraka zichukuliwe ili kudhibiti mimea inayohatarisha uoto wa asili katika Mamlaka ya Ngorongoro.
Katika kutatua changamoto hii, Waziri Makamba ameagiza kuundwa kwa jopo la wataalamu kutoka Tume ya Sayansi na Tecknolojia, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira, Hifadhi za Taifa za Tanzania, Wizara ya Kilimo na Mifugo na Mamlaka ya Ngorongoro ndani ya miezi sita kufanyika kwa utafiti wa kina wa kisayansi wa kubaini mbinu mpya ya kupambana na mimea hiyo vamizi inayotawala mimea inayotumiwa na wanyama.
Akizungumza katika kikao kilichojumisha Wahifadhi wa Mamlaka ya Ngorongoro na Wajumbe wa Baraza la wafugaji, Waziri Makamba amesikitishwa na kitendo cha Uongozi wa Mamlaka ya Ngorongoro kushindwa kuandaa mpango kabambe wa usimamizi wa hifadhi baada ya ule wa awali kuisha muda wake. Waziri Makamba ameuagiza uongozi wa Ngorongoro kuandaa mpango huo mapema na kuwa shirikishi. ” Mpango mtakoandaa hakikisheni kuwa unakuwa shirikishi kwa jamii inayozunguka na wadau na Taasisi muhimu likiwemo Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akizungumza na Uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro mara baada ya kutembelea eneo hilo kujionea changamoto za kimazingira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiongea na Baraza la wafugaji (hawapo pichani) katika Wilaya ya Ngorongoro. Wafugaji hao walimweleza Waziri kilio cha muda mrefu cha mradi wa Josho Wilayani hapo, Waziri Makamba ameutaka uongozi wa Mamlaka ya Ngorongoro na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira kuleta ufumbuzi mapema.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akizungumza na Uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro mara baada ya kutembelea eneo hilo kujionea changamoto za kimazingira.
No comments