Ndege ya ‘wanawake pekee’ kutoka Malawi kutua Tanzania
Shirika la ndege la Malawi, Malawi
Airlines, limetangaza kwamba linapanga kufanya safari ya ndege
itakayosimamiwa na wanawake pekee Alhamisi wiki hii.
Ndege hiyo itasafirisha abiria kutoka mji wa Blantyre hadi Dar-es-Salaam nchini Tanzania na itatua kwa muda Lilongwe kabla ya kuelekea Dar .
Taarifa kutoka kwa shirika hilo la ndege, lilisema lengo ni kufanikisha ulimwengu ambao "unakumbatia jinsia zote".
Ndege hiyo itakuwa chini ya Kapteni Yolanda Kaunda akisaidiwa na Lusekelo Mwenifumbo.
Bi Mwenifumbo, 24, alisomea taaluma ya uchukuzi wa ndege mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Ndege hiyo aina ya Bombardier Q-400 itapaa kutoka Blantyre saa nne asubuhi Alhamisi.
chanzo bbc
No comments