WAFANYAKAZI WASHAURIWA KUANZISHA VYAMA VYA KULINDA NA KUTETEA MASLAHI YAO
Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Uhifadhili Mahotelini na Majumbani kwa Huduma za Jamii na Ushauri (CHODAWA), Said Wamba akizungumza na waandishi wa habari wakati kongamano na baadhi ya matawi ya vyama wafanyakazi Dar es Salaam. (PICHA NA DALILA SHARIF)
Na Dalila Sharif
KATIBU Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Uhifadhili Mahotelini na Majumbani kwa Huduma za Jamii na Ushauri (CHODAWA), Said Wamba amezitaka Sekta za wafanyakazi zisizorasmi kujiunga kwa kuanzisha vyama vya wafanyakazi na taasisi binafsi ili kuweza kulinda na kutetea maslahi yao.
Akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano hilo la matawi ya vyama vya wafanyakazi (CHODAWO), Jijini Dar es Salaam leo alisema umuhimu wa vyama vya wafanyakazi ni kusaidia kulinda na kutunza maslahi ya wafanyakazi na wafanyabiashara ndogondogo.
Alisema wafanyakazi wengi na wafanyabiashara nchini wamekuwa hawajui kusimamia haki zao na kukabiliana na matatizo yanayowakabili katika shughuli zao za kukuza uchumi wa Taifa hilo.
“Wafanyakazi na wafanyabiashara wanatakiwa kuunda vyama kwa lengo la kuweza kuwatatulia matatizo yanayowakabili wanapokuwepo kazini na kukabiliwa na majanga au kudai haki ya kazi zake endapo amedhulumiwa , chama kinauwezo mkubwa wa kuwasilisha changamoto zao,”alisema Wamba.
Mratibu wa Shirikisho wa (CHODAWA) Vicky Kanyoka alisema kuwa wafanyakazi wanawake wa majumbani wa haki ya kusimamiwa haki zao katika kuwatetea na kuwasehea hivyo wapo baadhi ya waafanyabiashara wanawake hufanya kazi na kuanzisha baisahara bila kuwa na vyama na kushindwa kusimamia haki zao.
“Mifano mizuri nchini India wanawake wanashirikiana na kuwana muungano wa vyama vya wafanyakazi katika kutetea na kulinada maslahi yao katika ufanyaji kazi hali ambayo inawasaidia kuaendaelaea vyaema katika uazlishaji uchumi,”alisema Kanyoka.

No comments