Wanafunzi Wauguzi wa Chuo Kikuu cha Wright Jimbo la Ohayo Marekani Watembelea Chuo cha Afya na Sayansi za Tiba Mweni.
Kaimu
Mkuu wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba wa Chuo Kikuu cha Taifa cha
Zanzibar (SUZA) Amina Abdulkadir akizungumza na wanafunzi wauguzi wa
Chuo Kikuu cha Wright Jimbo la Ohayo nchini Marekani walipotembelea
Skuli hiyo Mbweni kubadilishana uzoefu.
Mwanafunzi
Muuguzi kutoka Chuo Kikuu cha Wright nchini Marekani Melissa Vanscoy
akieleza lengo la ziara yao hapa Zanzibar wakati wanafunzi wa vyuo
hivyo viwili walipokutana katika Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba ya
SUZA Mbweni.
Wanafunzi
wauguzi wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba ya SUZA wakibadilishana
mawazo na wanafunzi wenzao wa Chuo Kikuu cha Wright kutoka Jimbo la
Uhayo Marekani walipowatembelea skulini kwao Mbweni.
Wanafunzi
wauguzi kutoka Chuo Kikuu cha Wright na SUZA wakiwa katika darasa la
kufanyia mazoezi ya vitendo wakielekezana namna ya kumuhudumia mgonjwa
alielezwa wodini.
Picha ya pamoja
ya wanafunzi wauguzi wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba ya SUZA wakiwa
na baadhi ya walimu na wenzao wa Chuo Kikuu cha Wright, Jimbo la Uhayo
nchini Marekani wakiwa katika kempasi ya Mbweni.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar





No comments