WAZIRI NAPE AZIFAGILIA KURUGENZI YA MAWASILIANO IKULU NA IDARA YA HABARI MAELEZO KWA UBUNIFU NA WELEDI

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Nnauye (pichani) amezipongeza Kurugenzi za Mawasiliano ya Rais, Ikulu,
na
Idara ya Habari MAELEZO kwa ubunifu na weledi wanaouonesha katika
kuelezezea mafanikio ya Serikali kwa kutumia teknolojia mbalimbali za
habari na mawasiliano.
Waziri
Nape alisema licha ya changamoto ya vifaa vinavyowakabili Maafisa
Mawasiliano wa Serikali wamekuwa wanafanya kazi nzuri za kuisaidia
Sarikali ,amewataka kuwa wabunifu kwa kutumia teknolojia ya habari na
mawasiliano hasa mitandao ya kijamii katika kutekeleza majukumu yao
kwani ni nafuu na rahisi.
“Nawapongeza
sana wakurugenzi vijana Dkt. Hassan Abbasi wa MAELEZO na Greyson Msigwa
wa Ikulu. Hawa ni mfano wa ubunifu wa namna Serikali inavyoweza
kutumia teknolojia mbalimbali za mawasiliano katika kuhakikisha mazuri
yanayofanywa na Serikali yanatangazwa, yanaenezwa na kutetewa”alisema
Waziri Nape.
Waziri
Nape aliongeza kuwa pamoja na ubunifu wao katika mitandao ya kijamii,
utayarishaji wa makala za Serikali na kujibu hoja kwa haraka kupitia
taarifa kwa umma, wameweza pia kubuni vipindi vya TUNATEKELEZA na
SAFARI YA DODOMA ikiwa ni mkakati wa kusukuma mbele ajenda za Serikali.
Aidha,
Waziri Nape amewataka Maafisa Mawasiliano kutumia fursa zinazotolewa na
baadhi ya vyombo vya habari binafsi kupitia vipindi vya bure kwenye
Televisheni, redio na magazeti kuhakikisha mambo mazuri yanayotekelezwa
na Serikali yanatangazwa na kuweza kusikika kwa Wananchi.
“Nimezungumzia
hoja na haja ya mabadiliko kiutendaji, lakini nikiwa kiongozi ambaye
pia katika maisha yangu nimefanya kazi ya kuongoza kitengo cha habari na
uenezi nafahamu changamoto zinazoikabili kada hii,lakini unaweza
ukageuza changamoto kuwa fursa,kwahiyo tujiongeze ndugu zangu ” alisema
Waziri Nape.
Waziri
Nape alitoa wito kwa Makatibu Wakuu, Wakurugenzi,Wakuu wa Taasisi
pamoja na watendaji wakuu katika ofisi za umma kuhakikisha wanatenga
fedha katika bajeti kwaajili ya kununua vifaa vya kutendea kazi ili
kuviwezesha vitengo vya Mawasiliano Serikalini kutekeleza majukumu yake
kwa ufasaha na ufanisi katika kuisemea Serikali.
No comments