Siku hizi wasanii wakipigiwa simu wanaogopa kupokea – Kamanda Sirro
Kamanda wa polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema
kuwa kuna baadhi ya wasanii ambao hawapokei simu wakidhani wakipigiwa
itakuwa ni suala la dawa za kulevya.
Kamanda Sirro ameyasema hayo Jumatano hii katika mkutano wa Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ambapo leo ametimiza mwaka mmoja
tangu ateuliwe na Rais wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John
Pombe Magufuli.
Amesema, “Awali ya yote Kwanza nimpongeze Mkuu wa Mkoa wa Dar es
salaam, Paul Makonda kwa kutimiza mwaka mmoja lakini pia nimpongeze kwa
kuwaleta vijana wetu hasa wale waliokuwa wanatumia madawa ya kulevya.
Kwangu ni siku ya furaha kwasababu tangu hili zoezi lianze hata
nikiwapigia simu wasanii kama wakina Banana Zoro hawapokei simu, hata
viongozi wa dini hivyo hivyo lakini hii inaonesha kwamba kila mtu anajua
umuhimu wa suala hili.”
No comments