THURSDAY, MARCH 23, 2017 Kamati ya Bunge Yaipongeza Muhimbili kwa Kuboresha Huduma za Afya
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akitoa taarifa fupi ya utendaji kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii.ambayo imeitembelea hospitali hiyo leo. Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kingwangallah na Mwenyekiti wa kamati hiyo Peter Serukamba.
Baadhi ya Wajumbe wa kamati hiyo wakifuatilia ripoti ya utendaji iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Museru.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kingwangallah (kushoto), Mwenyekiti wa kamati hiyo, Peter Serukamba na Mkurugemzi Mtendaji wa MNH, Profesa Museru wakisiliza maoni ya wajumbe wa kamati hiyo leo.
Mjumbe wa Kamati hiyo, Dk Faustin Ndugulile akitoa maoni yake baada ya mkurugenzi wa hospitali hiyo kuwasilisha taarifa ya utendaji ya hospitali hiyo kwa wajumbe.
Baadhi ya wakurugenzi, wakuu wa idara wa hospitali hiyo wakifuatilia taarifa ya utendaji ya MNH iliyotolewa leo kwa wajumbe wa kamati hiyo.
Wajumbe wa kamati hiyo wakikagua jengo ambalo litatumika kutoa tiba kwa wagonjwa wa figo.
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Juma Mfinanga akiieleza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii jinsi huduma ya telemedicine inavyofanya kazi baada ya kuunganishwa na hospitali nyingine za mikoa. Kushoto ni Mwenyekiti wa kamati hiyo Peter Serukamba, Mjumbe Joseph Mbilinyi (katikati), Mjumbe Mussa Hassan Zungu na Zitto Kabwe
No comments