WASOMI WAPONGEZA USAWA WA JINSIA UMOJA WA AFRIKA(AU)
Mwandishi Wetu,Arusha
Wasomi
nchini wamepongeza uteuzi wa majaji wawili wanawake wa Mahakama ya
Afrika na Haki za Binadamu(AfCHPR)uliofanywa na Wakuu wa Umoja wa
Afrika(AU) katika mkutano wa 28 uliofanyika nchini Ethiopia kuwa
unaelenga kujenga usawa wa kijinsia katika chombo hicho cha maamuzi.
Mkutano
huo pamoja na mambo mengine ulipitisha majina ya majaji wawili ambao ni
Jaji Bensaoula Chafika kutoka Algeria na Jaji Chizumila Rose Tujilane
wa Malawi ambao wataitumikia mahakama hiyo kwa kipindi cha miaka sita
ijayo.
Majaji
hao wanachukua nafasi zilizoachwa wazi na Jaji Fatsah
Ouguergouz(Algeria) na Jaji Duncan Tambala(Malawi)ambao utumishi wao
ulikoma tangu Septemba 5,2016.
Mhadhiri
Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Sebastian Kolowa Memorial(Sekomu),Dk
Happiness Rwejuna aliyewaongoza wanafunzi wa sheria kutembelea Mahakama
hiyo yenye makao yake jijini hapa alisema uamuzi uliofanywa na AU ni
mzuri na ufaa kuigwa na nchi wanachama katika uteuzi wa wanawake wenye
uwezo katika nafasi za maamuzi.
“Naamini
idadi ya wanawake wenye elimu ya juu wapo wengi na wanaweza kufanya
kazi kwa umahiri mkubwa,isihishie katika ngazi ya AU tuu bali ishuke
hadi kwa nchi moja moja kuona wanawake wana mchango muhimu katika
maendeleo ya Afrika kwa ujumla,”alisema.
Majaji
hao wanatarajiwa kuapishwa katika kikao cha 44 kinachotarajiwa
kufanyika Machi 6,2017 jijini Arusha ikiwa ni mara ya kwanza kwa
mahakama hiyo kuwa na majaji wanawake watano katika majaji 11 wa
mahakama hiyo tangu ianze kazi zake mwaka 2004.
Naye
Emmanuel Chipanta mwanafunzi wa mwaka tatu alisema uwepo wa mahakama
hiyo una umuhimu katika kuimarisha utawala sheria kwani kumekua na
makosa mengi yanayotendeka ambayo wahusika hawana budi kukabiliana na
mkondo wa sheria.
Alisema uwiano wa kijinsia unatajwa katika itifaki iliyoanzisha mahakama hiyo katika ibara ya 12(2) na Ibara ya 14(3).
Kwa
upande wake Mwanasheria wa Mahakama hiyo,Selemani Kinyunyu wakati
akijibu hoja za wanafunzi hao waliotaka kufahamu uamuzi wan chi za
Afrika kutaka kujiondoa katika Mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai
alisema sula hilo lina sura mbili katika nchi zinazotaka kujiondoa na
zinazotaka kubaki.
“Zipo
nchi zinazoona mahakama hii imekua ikiwalenga viongozi wa Afrika zaidi
badala ya kushughulikia jinai ulimwenguni kote hivyo kuona hamna sababu
ya kuendelea kuwa mwanachama,lakini wapo wanaodhani ni muhimu kuendelea
kuwepo ili kuotoa mapendekezo ya maboresho pale penye mapungufu jambo
ninaloliunga mkono,”alisema
Afisa
Uhusiano Mwandamizi wa Mahakama ya Afrika na Haki za
Binadamu(AfCHPR)Sukhdev Chhatbar akizungumza na wanafunzi wa mwaka wa
tatu kozi ya sheria katika Chuo Kikuu cha Sebastian Kolowa
Memorial(Sekomu)kilichopo Lushoto mkoa wa Tanga wakati wa ziara ya
masomo katika mahakama hiyo mkoani Arusha.Picha na Filbert Rweyemamu
Afisa
Uhusiano Mwandamizi wa Mahakama ya Afrika na Haki za
Binadamu(AfCHPR)Sukhdev Chhatbar akizungumza na wanafunzi wa mwaka wa
tatu kozi ya sheria katika Chuo Kikuu cha Sebastian Kolowa
Memorial(Sekomu)kilichopo Lushoto mkoa wa Tanga wakati wa ziara ya
masomo katika mahakama hiyo mkoani Arusha.
Wafanyakazi
na wanafunzi wa sheria katika Chuo Kikuu cha Sebastian Kolowa
Memorial(Sekomu)kilichopo Lushoto mkoa wa Tanga wakiwa kwenye chumba cha
mahakama ya wazi katika Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu(AfCHPR)
wakati wa ziara ya mafunzo.



No comments