WAANDISHI WA HABARI ZA BUNGE WAJENGEWA UWEZO KUHUSU SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI NA HAKI YA KUPATA TAARIFA NA WAJIBU WAO JUU YA SHERIA HIZO
Taasisi
ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania kwa
kushirikiana na Wakifu wa Taasisi Huru za Uwazi Afrika (OSIEA)
wamefanya semina ya siku moja na waandishi wa habari mkoani Dodoma
katika ukumbi wa Hazina Ndogo, iliyolenga kuboresha utendaji katika
kazi zao.
Mjadala
huu umelenga kuwajengea wanahabari uwezowa utendaji wao wa
kazi.Waandishi wa habari hao wamejengewa uwezo kuhusu sheria ya huduma
zavyombo vya habari ili kuleta ufanisi katika majukumu yao. Mkutano huu
umefanyika katika ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma.
Mhariri
mtendaji wa Jamhuri Media, Deodatus Balile akitoa mada kwa wanahabari
waliofika kwenye semina iliyokuwa ikihusu utendaji kazi wao wa kila
siku.
Wakili
wa Mahakama Kuu na Mhariri wa Zamani, James Marenga akitoa mada
inayohusisha sheria mbalimbali zinazohusiana na waandishi wa habari na
namna ya kufanya kazi bila kuvunja sheria zilizowekwa.
Afisa
Habari na Utafiti wa MISA-Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa akizungumza
jambo kwenye semina ya Wanahabari uliofanyika katika ukumbi wa Hazina
Ndogo mjini Dodoma leo.
Mhariri
Mtendaji wa The Guardian Ltd, Jesse Kwayu akizungumza jambo kwenye
semina iliyowakutanisha wanahabari mbalimbali waliokutanishwa na Misa
Tanzania ili kujadili changamoto zinazowapata katika kazi zaohasa za
bungeni.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakichangia mada pamoja na kuuliza maswali kwa
watoa mada waliowasilisha mada mbalimbali katika ukumbi wa Hazina Ndogo
mjini Dodoma.
Baadhi
ya waandishi wa habari waliofika katika semina iliyoandaliwa na Misa
Tanzania kujadili namna ya kufanyakazi kifanisi katika majukumu yao ya
kila siku
Picha ya pamoja
No comments