IDADI KUBWA YA WAKAZI WA WILAYA YA IGUNGA WAPO HATARINI KUPAMTWA NA MAGONJWA YA SHINIKIZO LA DAMU
Jengo
la Ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora
kulikofanyikia zoezi la upimaji wa afya kwa watumishi wa Halmashauri ya
wilaya ya Igunga,Madiwani wa Halmashaurri hiyo pamoja na wananchi wa
Halmashauri waliojiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF).
Na Jumbe Ismailly, Igunga
IDADI
kubwa ya wananchi wa Wilaya ya Igunga, Mkoani Tabora wapo hatarini
kupatwa na magonjwa ya shinikizo la damu kutokana na kutokuwa na
utamaduni wa kupima afya zao hali ambayo inachangia miili yao kuwa na
uzito mkubwa kupita kiasi.
Mganga
Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Dk. Godfrey Mgongo aliyasema hayo wakati wa
zoezi la kupima afya kwa watumishi,madiwani pamoja na wananchi ambao ni
wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya (NHIF) wa Halmashauri ya
wilaya hiyo lililofanyika kwenye viwanja vya Ofisi za Halmashauri hiyo.
Baadhi
ya wataalamu wa sekta ya afya waliokuwa wakitoa huduma za upimaji afya
kwa watumishi wa Halmashauri ya Igunga,Madiwani pamoja na wananchi wa
kawaida waliojiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF)ambapo
iligundulika kuwa idadi kubwa ya wakazi wake wapo hatarini kupatwa na
magonjwa ya shinikizo la damu kutokana na kutokuwa na utamaduni wa
kupima afya zao na hivyo kuchangia miili yao kuwa na uzito mkubwa kupita
kiasi.
“Kitu
ambacho tumekigundua ni kwamba watumishi wengi au watu wengi wana uzito
uliopitiliza,uzito mkubwa na hii inaweza ikapelekea ukapata magonjwa
ambayo yatawaathiri katika maisha yao”alisema Dk.Mgongo.
Hata
hivyo mganga mkuu huyo wa wilaya alivitaja vitu vilivyopimwa na
wataalamu hao kutoka shirikisho la vyama vya magonjwa yasiyokuwa ya
kuambukiza(TANCDA) kuwa ni uzito,shinikizo la damu,homa ya ini pamoja na
kisukari na zoezi hilo limefanyika kwa siku nne ambapo lilianza kwa
watumishi wa Halmashauri na baadaye huduma hiyo ilielekezwa kwa madiwani
pamoja na wananchi.
Baadhi
ya Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora wakiwa
kwenye mkutano wa Baraza la kawaida la madiwani wa Halmashauri hiyo
ambalo lilitumika pia kushiriki katika zoezi la upimaji afya kwa
waliojiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF).(Picha Na Jumbe
Ismailly)
Kwa
mujibu wa Dk.Mgongo kati ya zaidi ya watumishi 60 wa Halmashauri hiyo
waliopatiwa huduma ya upimaji wa afya, imegundulika kuwa tatizo kubwa
linalowakabili watumishi hao ni uzito ingawa kuna tatizo la homa ya ini
na ugonjwa wa kisukari ndiyo unaofuatia.
“Lakini
pia kwa waheshimiwa Madiwani kuanzia asubuhi mpaka sasa wameshapimwa
madiwani 61 na imegundulika kwamba robo tatu ya waliopima wanakabiliwa
na tatizo la kuwa na uzito mkubwa kupitiliza,kisukari na homa ya ini
vina asilimia ndogo sana”alisisitiza Mganga mkuu huyo wa wilaya.
Kuhusu
madhara yatokanayo na uzito mkubwa kupitiliza,Dk,Mgonga hata hivyo
aliyataja kuwa ni pamoja na shinikizo la damu,kisukari na magonjwa
mengine yanayotokea baada ya kupata magonwa hayo na endapo ugonjwa mmoja
ukitatuliwa unasaidia kuzuia magonjwa mengine mengi yanayoweza kutokea.
Akitoa
ushauri kwa watumishi,wananchi na madiwani wanachama waliohudhuria
katika zoezi hilo la kupima afya zao,Mganga Mfawidhi,Bi Elizabeth
Mpangala aliwashauri wananchi hao kupunguza matumizi ya chakula kwani
kwa kufanya hivyo kutasaidia pia uzito kupungua.
Aidha
Bi Mpangala aliwasisitiza pia kwamba wazidishe matumizi ya mboga za
majani,vyakula vya protini pamoja na kufanya mazoezi kutasaidia
kupunguza uzito huku akionyesha kutoridhishwa na baadhi ya watu
kutotumia mboga za majani ambazo zina sukari ndogo,tofauti na wanga na
vyakula vyenye protini.
Naye
diwani wa kata ya Iborogelo,Bwana Simbalugombi Ndali aliweka bayana
kwamba baada ya kushiriki katika zoezi hilo la kupima afya aligundulika
kuwa na kilo 93 na hivyo kutumia fursa hiyo kutoa wito kwa wananchi
kuhakikisha wanafuata ushauri wa wataalamu wa afya ili kukabiliana na
magonjwa hayo yanayotokana na kuwa na uzito mkubwa kupitiliza.
No comments