DC SHINYANGA AKABIDHI VIFAA TIBA VILIVYOTOLEWA NA WATANZANIA WAISHIO DENMARK KWA AJILI YA WANANCHI WA SHINYANGA
Hapa
ni katika viwanja vya Ofisi ya Mtendaji Kata ya Ngokolo katika manispaa
ya Shinyanga ambapo leo Jumamosi Februari 11,2017 Mkuu wa wilaya ya
Shinyanga Josephine Matiro amekabidhi vifaa tiba kwa mkurugenzi wa
manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kuvisambaza katika zanahati na
hospitali zilizopo katika manispaa hiyo.
Vifaa
tiba hivyo vimetolewa na Watanzania waishi nchini Denmark ambapo
upatikanaji wa vifaa hivyo unatokana ushirikiano wa Diwani wa kata ya
Ngokolo Emmanuel Ntobi (CHADEMA) na shirika la AGAPE la Mjini Shinyanga
kuwasiliana Watanzania waishio nchini Denmark kisha kuleta vifaa hivyo.
Akizungumza
wakati wa makabidhiano hayo,Mkurugenzi wa shirika la AGPAE John Myola
alisema wazo la kutafuta vifaa tiba lilitolewa na diwani wa kata ya
Ngokolo Diwani Emmanuel Ntobi ambaye anajuana na watanzania waishio
nchini Denmark.
“Diwani
huyu alitupatia mawasiliano ya watu hao wanaojulikana Denish Relief
Group kisha sisi kama shiriki tukaandika andiko tukiomba kupewa vifaa
tiba kwa ajili ya kupunguza uhaba wa vifaa tiba katika zahanati na
hospitali za manispaa ya Shinyanga”,alisema Myola.
Myola
alitumia fursa hiyo kuiomba ofisi ya mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga
kuhakikisha kuwa vifaa tiba hivyo vinatumika kama inavyotakiwa na
kuhakikisha vinatunzwa.
Naye
Diwani wa kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi alisema watanzania waishio
Denmark wametoa vifaa tiba hivyo bure kwa ajili ya watanzania huku
akiishukuru serikali kuruhusu vifaa hivyo kuingia nchini bila kulipiwa
kodi.
“Hili
jambo la kidiplomasia kwa nchi hizi mbili Tanzaia na Denmark,Denish
Relief Group ni kundi la watu la kwanza kutoa msaada mkubwa nchini,huu
ni kama mwanzo tu,wamesema wataendelea kutoa msaada na wamesema wapo
tayari kutujengea zahanati katika kata hii ya Ngokolo ambayo haina
zahanati”,alisema Ntobi.
“Tumepokea
vifaa tiba aina 26,vimo vitanda,magodoro,viti vya kisasa vya
wagonjwa,mashine ya Utra sound,mashine ya Incubation na vifaa vingine
vingi ambavyo vitatumika katika kutoa huduma za afya kwa wananchi wa
manispaa ya Shinyanga”,aliongeza Ntobi.
Hata hivyo diwani huyo aliomba vifaa hivyo vitumike vizuri na vitumike kwa wananchi wenye kipato cha hali ya chini.
Alisema
pamoja na kutoa vifaa tiba,pia watanzania hao waishio nchini Denmark
wametoa baiskeli kwa watu wenye ulemavu na nguo kwa makundi ya watu
wasiojiweza wakiwemo wazee wanaolelewa katika kituo cha Kolandoto
kilichopo katika manispaa ya Shinyanga.
Kwa
upande wake mgeni rasmi katika makabidhiano hayo,Mkuu wa wilaya ya
Shinyanga Josephine Matiro alipongeza jitihada zilizofanywa na shirika
la AGAPE na diwani wa kata ya Ngokolo katika kupatikana kwa vifaa
hivyo.
“Hili
ni tukio kubwa na la busara sana,limetutia moyo ,nawapongeza sana
watanzania waishio Denmark na wote mliofanikisha kupatikana kwa vifaa
hivi ambavyo vitakuwa msaada mkubwa kwa wananchi,huu siyo muda wa
kufanya siasa,kinachotakiwa ni kuwaletea maendeleo wananchi bila kujali
itikadi za kichama”,alieleza Matiro.
“Katika
suala la maendeleo,serikali ipo tayari kushirikiana na shirika,kundi
lolote la watu na hata mtu binafsi,tusitumie majukwaa ya maendeleo
kufanya siasa,nimpongeze diwani wa kata hii kwa ushirikiano aliotuonesha
katika kuwasaidia wananchi”,aliongeza Matiro.
Vifaa
tiba vilivyotolewa na watanzania waishio nchini Denmark kwa ajili ya
kusaidia kutoa huduma za afya katika zahanati na hospitali zilizopo
katika manispaa ya Shinyanga
Vifaa vya kufanyia mazoezi na viti vya kubebea wagonjwa
Vifaa tiba mbalimbali ikiwemo magongo,viti vya kuogea
Vifaa tiba vikiwa katika viwanja vya ofisi ya Afisa mtendaji kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga
Baiskeli za wagonjwa na vifaa tiba vingine vya kisasa
Vitanda vya wagonjwa
Vitanda vikiwa na magodoro yake
Afisa
Mtendaji wa kata ya Ngokolo William Ndila akitambulisha wageni
mbalimbali waliohudhuria hafla fupi ya kukabidhi vifaa tiba
vilivyotolewa na watanzania waishio nchini Denmark "Denish Relief Group"
kutokana na jitihada zilizofanywa na diwani wa kata hiyo Emmanuel Ntobi
na Shirika la AGAPE
Mkurugenzi wa shirika la AGAPE la Mjini Shinyanga John Myola akizungumza katika hafla hiyo
Wananchi wakiwa eneo la tukio
Aliyesimama
ni Mkurugenzi wa shirika la AGAPE la Mjini Shinyanga John Myola
akielezea namna vifaa tiba vilipatikana kwa ajili ya kusaidia kutoa
huduma za afya kwa wananchi wa manispaa ya Shinyanga
Diwani
wa kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga Emmanuel Ntobi(Chadema)
akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba hivyo.Kushoto ni
diwani wa viti maalum Zainab Heri (Chadema).Kulia ni mkuu wa wilaya ya
Shinyanga Josephine Matiro
Wananchi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Diwani
wa kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga Emmanuel Ntobi(Chadema)
aliwashukuru viongozi wa serikali kwa kuruhusu vifaa tiba hivyo kuingia
nchini bila kodi huku akiomba serikali kuwapatia eneo kwa ajili ya
kujenga zahanati katika kata hiyo ambayo haina zahanati kutokana na
kushindwa kujenga baada ya kuibuka mgogoro kwenye eneo ambapo kulitakiwa
pajenge zahanati
Kaimu
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Magendi Magenzi ambaye ni afisa
utumishi wa manispaa hiyo,akizungumza katika hafla hiyo ambapo kwa namna
ya pekee alimpongeza diwani wa kata ya Ngokolo kwa jitihada alizofanya
katika upatikanaji wa vifaa tiba hivyo.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Ngokolo John Nangi akizungumza wakati wa hafla hiyo
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa hafla hiyo
ambapo alisema serikali inaunga mkono jitihada zinazofanywa na wadau
mbalimbali katika kuwaletea maendeleo wananchi
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika hafla hiyo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisisitiza umuhimu wa kuendeleza siasa kwenye masuala ya maendeleo
Diwani
wa kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi akimwonesha mkuu wa wilaya vifaa tiba
hivyo ikiwemo vifaa vya kubebea watoto na vifaa vya kufanyia mazoezi
Diwani
wa kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi akiendelea kumwonesha mkuu wa wilaya
ya Shinyanga vifaa tiba,pichani ni meza za kulia chakula na kabati
Diwani wa kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi akionesha vifaa tiba
Diwani wa kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi akiwa ameshikilia fimbo za watu wasioona
Baada
ya kukabidhi baiskeli kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa viungo,Mkuu wa
wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akishikana mkono na Richard ambaye
ni mlemavu wa viungo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisalimiana na kijana mwenye ulemavu wa viungo baada ya kumkabidhi baiskeli
Wananchi wenye ulemavu wa viungo wakiwa wamekaa kwenye baiskeli
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na mkurugenzi wa shirika la
AGAPE John Myola wakiwasindikiza wananchi wenye ulemavu wa viungo baada
ya kuwapatia baiskeli hizo.Baiskeli hizo zinaendelea kutolewa kwa
wananchi mbalimbali wenye ulemavu wa viungo
Mashine ya Utra Sound ambayo pia imetolewa na watanzania waishio Denmark
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza baada ya kuona
mashine mbili Utra Sound kwa ajili ya akina mama wajawazito na Mashine
ya kukuzia watoto njiti
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza baada ya kuona mashine za kisasa za kutolea huduma za afya
Picha zote na Kadama Malunde
No comments