MAMLAKA YA UDHIBITI NA MANUNUZI YADHAMIRIA KATIKA KUBORESHA MANUNUZI YA ZABUNI
MAMLAKA wa Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA)imejizatiti katika kufanya marekebisho ya sheria ikiwa ni katika kuboresha zaidi manunuzi ya zabuni kwa serikali.
Akizungumza
wakati akitembelea banda la PPRA lililopo kwenye jengo la Wizara ya
Fedha na Mipango, Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA Dkt Laurent Shirima
amesema kuwa maboresho hayo yatalenga katika sehemu tano ambazo
zitaboresha manunuzi ya zabuni katika nyanja mbalimbali.
Dkt
Shirima amesema kuwa wataboresha manunuzi katika kupunguza gharama za
ununuaji wa zabuni, serikali kununua kwa bei za sokoni wakimaanisha bei
halisi ya zabuni pia watatoa upendeleo kwa makampuni ya ndani ikiwemo
makundi maalumu kama vile wanawake, wazee na vijana.
Ameongezea
kuwa, katika maboresho mengine yatakuwa ni katika kuendeleza viwanda
kama serikali ya awamu ya tano inavyosisitiza ukuaji wa viwanda huku
PPRA ikiangalia zaidi wataalamu wa manunuzi kutoka ndani pia wapo katika
hatua za mwisho za kuhamia katika mfumo wa kieletroniki wa ununuzi wa
zabuni.
PPRA
ni mamlaka inayohusiana na udhibiti wa manunuzi ya Umma ambapo kupitia
kwa Mtendaji Mkuu Dkt Shirima amewaondoa hofu wananchi kuwa waiamini
taasisi yao kwani mambo mengi ya msingi yameshawekwa wazi na fedha za
umma zinahitaji uwajibikaji.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka wa Udhibiti wa Manunuzi ya Umma PPRA Dkt
Laurent Shirima akizungumza na wanahabari wakati alipotembelea banda la
Mamlaka wa Udhibiti wa Manunuzi ya Umma PPRA lililopo kwenye jengo la
Wizara ya Fedha na Mipango na kuelezea namna wanavyojizatiti katika
kuboresha ununuaji wa zabuni kwa serikali.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka wa Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) Dkt Laurent Shirima akimuhudumia mwananchi aliyetembelea banda lao na katika maadhimisho ya 41 ya Monesho ya kimataifa ya Sabasaba leo Jijini Dar es salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka wa Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA)
Dkt Laurent Shirima akipata maelezo kutoka kwa mfanyakazi wa Mfuko wa
Pensheni wa Taifa (PPF) wakati alipotembelea banda hilo lilipo katika
Jengo la Wizara ya Fedha na Mipango katika maadhimisho ya 41 ya Monesho ya kimataifa ya Sabasaba leo Jijini Dar es salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka wa Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA)
Dkt Laurent Shirima akisaini katika kitabu cha wageni wa Wizara ya
Fedha na Mipango alipotembelea banda hilo katika maadhimisho ya 41 ya
Monesho ya kimataifa ya Sabasaba leo Jijini Dar es salaam.
Afisa
Mahusiano Mwandamizi wa Mamlaka wa Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA)
Mcharo Mrutu akimuhudumia mwananchi aliyetembelea banda lao katika
maadhimisho ya 41 ya Monesho ya kimataifa ya Sabasaba leo Jijini Dar es
salaam
Mtaalamu wa Mifumo ya Habari wa Mamlaka
wa Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) Mapinduzi Muhochi akitoa elimu
ya manunuzi ya zabuni kwa mwananchi aliyejitembelea banda
lao katika maadhimisho ya 41 ya Monesho ya kimataifa ya Sabasaba leo
Jijini Dar es salaam. Picha Zote na Emannuel Massaka.
No comments