JAFO AKEMEA TATIZO LA MIMBA KWA WANAFUNZI WILAYA YA UKEREWE.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi
Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya sekondari wasichana
ya Bukongo wilayani Ukerewe.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani
Jafo akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya sekondari ya
wavulana ya kidato cha tano na sita ya
Pius Msekwa wilayani Ukerewe.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani
Jafo akizungumza na watumishi wa Halmashuari ya wilaya ya Ukerewe wakati
akihitimisha ziara yake wilayani humo.
Watumishi wa halmashauri ya Ukerewe
wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo.
.................................................................................
Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo
amekemea tatizo la wanafunzi wa sekondari kupata mimba wakiwa shuleni ambapo
hadi sasa kuna wanafunzi 108 ambao wamebainika kuwa na ujauzito kwenye wilayani
Ukerewe.
Kauli hiyo ameitoa katika ziara yake ya kukagua miradi ya
maendeleo kwenye sekta mbalimbali wilayani humo.
Jafo amewataka viongozi wote wilayani humo kuungana kupambana na
tatizo hilo bila ya kuoneana aibu.
Naibu Waziri huyo amewataka wanafunzi kuzingatia masomo kwani
elimu ndio msingi wa maisha kwa mwanadamu yeyote.
Amewakemea wanafunzi wakike wenye tabia ya kujihusisha kwenye
mapenzi wakiwa na umri mdogo na kwamba jambo hilo linahatarisha mustakabali wa
maisha.
Katika ziara hiyo,Jafo alifanya ukaguzi wa ujenzi wa mabweni,
madarasa, maabara, na vyoo kwa shule ya sekondari Pius Msekwa na sekondari ya
Bukongo ambapo serikali ilipelekwa fedha mwezi April mwaka huu zaidi ya sh.
milioni 500 ili kuwezesha elimu ya kidato cha tano na sita wilayani humo.
Naibu Waziri Jafo amemaliza ziara yake wilayani Ukerewe mkoani Mwanza na kuelekea wilaya na Tarime na Rorya mkoani Mara.




No comments