MAADHIMISHO YA MIAKA 100 YA CHAMA CHA SKAUTI NCHINI TANZANIA YAFANA DODOMA.
![]() |
| Makamu wa Rais Samia Suluhu akiwa anazungumza katika maadhimisho ya miaka 100 tangia kuanzishwa kwa uskauti nchini mwaka 1917-2017.Picha na Vero ignatus Blog |
Pichani ni baadhi ya Skauti wakiwa wameshikilia bango wakiwa katika maeneo ya Chuo Kikuu cha Dododma katika maadhimisho ya chama hicho kutimiza miaka 100.Picha na Vero Ignatus Blog.
Katika picha ni baadhi ya Skauti kutoka katika halmashauri zote hapa nchini na katika mikoa yote nchini wakiwa nje ya ukumbi wakisubiria kuingia ndani ya ukumbi.Picha na Vero Ignatus Blog
![]() |
![]() |
Skauti
wakiwa ukumbi wa Chimwaga Chuo Kikuu Dodoma wakiwa wanafurahia katika
sherehe ya kuadhimisha miaka 100 tangia kuanzishwa kwa uskauti nchini
Tanzania .Picha na Vero Ignatus Blog.
Makamu
wa Rais mama Samia Suluhu akimvisha nishani Rais msataafu wa awamu ya
pili Alhaji Ally Hassan Mwinyi9 1985-1995)Katika maadhimisho ya miaka
100 tangia kuanzishwa kwa uskaunti nchini.![]()
|

Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu akimvisha nishani Rais mastaafu wa ZANZIBAR Aman Abeid Karume ambaye pia alikuwa mlezi wa Skauti .

Waziri mkuu mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim akivishwa nishani ambapo amekuwa skauti tangia shuleni ,hata alipokuwa Katibu mkuu wa nchi huru za Afrika ambapo mwaka 2001 alipendekeza kuwa kilanchi huru ya Afrika iwe na siku yake ya kuadhimisha siku ya Skauti Afrika ambapo hufanyika kila mwaka tarehe 13 march ambapo hapa nchini ilisheherekewa Jijini Arusha
| Skauti wakiwa maeneo ya Chuo kikuu Dodoma wakiwa wanasubiria sherehe ya kkuadhimisha miaka 100 ya chama cha skauti tangia kuanzishwa nchini Tanzania mwaka 1917-2017.Picha na Vero Ignatus Blog. |
Maadhimisho ya miaka 100 tangia kuanzishwa kwa uskauti nchini Tanzania mwaka 1917 yamefanyika leo Mkoani Dodoma ambapo mgeni rasmi alikuwa makamu wa Rais Samia Suluhu ambaye alimuwakilisha Rais Dkt John Magufuli,ambapo yamebeba kauli mbiu isemayo kuwajenga vijana kuwa wazalendo kwa maendeleo ya Jamii.
Maadhimisho hayo yamewashirikisha Skauti kutoka katika halmashauri zote katika mikoa yote nchini sambamba na nchi mbalimbali ikiwemo Kenya,Uganda,Rwanda,Kongo,na Komoro ambapo hapo awali walianza skauti 850 kwa sasa Tanzania wapo zaidi ya 400,000 duniani pote wakiwa skauti zaidi ya 4,000,000
Akizungumza katika maadhimisho hayo Makamu wa Rais amewataka wazazi kuwaruhusu watoto wao kujiunga kwa wingi katika vilabu vilivyopo mashuleni ili kujijengea uwezo ,ukakamavu,maadili na nidhamu kwani wakilelewa vizuri katika skauti watakuja kuwa viongozi wazuri wenye mfano bora wa kuigwa.
Aidha amewataka Skauti wote nchini kuyatenda matendo mema yatakayoandikwa katika historia nzuri maishani mwao kwani moja ya jukumu la skauti ni ukakamavu,malezi bora,uzalendo na kulipenda Taifa lao.
Maadhimisho hayo ya miaka 100 tangia kuanzishwa kwake mwaka 1917-2017 hapa nchini yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo marais wastaafu kutoka Tanzania Bara na Visiwani .






No comments