WAZIRI NCHEMBA: MADEREVA WANAOACHA MAWE BARABARANI BAADA YA MATENGENEZO WACHUKULIWE HATUA KALI
Na Vero Ignatus.Singida.
Waziri wa
mambo ya ndani Mwigulu Lameck Nchemba ameliagiza jeshila polisi kitengo cha usalama
barabarani kuwachukulia hatua kali za kisheria madereva ambao magari yao yanaharibika njiani
wanaacha mawe makubwa baada ya matengenezo ya magari hayo
"Nawaagiza jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani chukueni alama na namba za magari yao haijalishi watakuwa wamevuka mikoa mingapi warudisheni waje wayaondoe mawe yao waliyoyaacha barabarani"alisema waziri.
Amesema leo katika ziara ya Rais Dkt.Magufuli mkoani Singida alipopewa nafasi ya kusalimia wananchi ambapo amesema kuwa kuwa jukumu la utunzaji wa
barabara ni la kila mtu na siyo serikali peke yake hivyo ni vyema wananchi
wakaelewa kuwa utengenezaji wa barabara umetumia kiasi kikubwa cha fedha.
"wakati utengenezaji wa barabara unapoeendelea kila mtu anatamani iishe mapema ili itumike ,lakini wanasahau kuwa wanahitajika kuitunza ,kila mtu atunze barabara kwa maslahi ya Taifa letu"alisisitiza waziri.
Aidha
amewataka madiwani wote kuwasaidia na kuwaelimusha jamii ya wafugaji namna ya
kutumia vivuko vya wanyama vilipo na wavitumie ipasavyo ili wanyama wasiaharibu
barabara.
"Tumuunge rais mkono katika juhudi zake ananzozifanya za kuleta maendeleo katika nchi hii"alisisitiza.
No comments