DKT MAGUFULI:KIONGOZI AMBAE HATAAMASISHA WATU WAKE KILIMO HAFAI KUWA KIONGOZI

 
Na.Vero Ignatus Singida 

Ikiwa leo ni siku ya kumbukumbu mashujaa waliopigana vita ya Kagera 1978-1979 hapa nchini, Rais John Magufuli amezindua barabara ya mji mdogo Itiji- Chaya mkoani Singida yenye urefu wa kilometa 89.3 ambapo barabara hiyo pia itawarahisishia safari wasafiri wa mikoa ya Singida na maeneo ya jirani kuelekea mkoa wa Tabora mpaka Kigoma.
Katika uzinduzi huo Rais ameyapongeza majeshi yote hapa nchini pamoja na mashujaa wote waliopambana hadi kuiweka Tanzania mahali ilipo sasa ambapo amewataka wananchi wote kulinda na kutunza Amani kwani palipo na Amani ndipo penye mafanikio ya kweli.
"Nawaombeni watanzania muilinde amani iliyopo kwani palipo na amani   tutafanikiwa,palipo na amani tutafanya yote,niwaombe muwe na mioyo ya kuvumiliana"alisema Rais.

Aidha ametoa angalizo kwa wakuu wa wilaya,mikoa,tarafa pamoja na vijiji nakusema kuwa Serikali haitatoa chakula kwa mkoa utakaokumbwa na baa la njaa na badala yake viongozi wa mkoa huo watawajibishwa na kuonekana hawafai kuwa viongozi.

"Nasema hivi Kiongozi ambaye hatahamasisha watu wake kulima hafai kuwa kiongozi wilaya ikiwa na njaa nitajua wewe mkuu wa mkoa hufai, mkuu wa wilaya hufai. Mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya atakayeshindwa kuwahamasisha watu wake wafanye kazi, hafai kuwa kiongozi,”alisisitiza.

Amewaagiza wakuu wa mikoa kuwaondoa katika nafasi zao makatibu tarafa ambao hawahamasishi kilimo kwa wananchi
“Ikiwezekana na wewe mkuu wa wilaya au mkoa, kama unakaa kijijini au ni katibu kata onyesha mfano wako wa kazi, Ukiwa diwani, hivyo hivyo, ukiwa mbunge hivyo hivyo,  Ndiyo maana ninatimiza wajibu wangu wa kuhamasisha watu, chapa kazi, hapa kazi tu.” Amesema.
Ameitaka  Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) ambao wapo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,kupitia upya bei ya ujenzi wa barabara kutoka Chaya hadi Nyaua waweke mapatano upya wa ujenzi wa barabara hiyo kwani kiasi walichokiweka cha shilingi bilioni 104 ni kikubwa kwa ujenzi wa kilometa 57.

''Zungumzeni na huyo mkandarasi akikubali kuijenga hiyo barabara isiwe lilometa 57 peke yake ila mumuongezee,akikataa mkateni hiyo pesa,nawaambia wizara ambayo sijatoka ni wizara hii ya Ujenzi ninaichungulia kwa mbali ,hatuhitaji wakandarasi wanaokuja kufanya biashara hapa,tunahitaji matumizi sahihi ya pesa."alisema Rais.
Sambamba na hayo amesema kuwa kwasasa yeye ndiye Rais na anafanya marekebisho ya yale mabaya yaliyotendeka huku akisisitiza kuwa hwenda ikawa atakapomaliza kipindi chake cha uongozi asitokee atakayekemea .
''kama kuna makosa yaliyofanyika machache lazima tuyarekebishe, tufike mahali tutoshe ,ukiona watu wanapiga kelele kwa kupinga hili ujue amemeza chochote na alichomeza ujue ni rushwa aliyopewa,usikosee kuchagua madhara yake ni makubwa sana"alisema.

No comments