KAMATI YA MAADILI YA MADIWANI YATOA TAARIFA

ARUSHA

Kamati ya maadili ya madiwani ambayo ilikuwa imepewa jukumu la kufuatilia malalamiko ya diwani wa kata ya Mwandeti Bwana Boniface Tarakwa akimlalamikia Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha DC Bwana Naoh Lembris imetoa taarifa yake kuhusu walioyabaini.

Wakieleza mbele ya kikao cha baraza la madiwani kamati hiyo ilipokea malalamiko kutoka kwa Bwana Boniface kwamba mwenyekiti wa halmashauri amemwita mnafiki na anapaswa kuombewa katika mkutano wa baraza .

Hata hivyo kamati hiyo ilipokea malalamiko ya mwenyekiti wa halmashauri Bwana Noah Lembris akimlalamikia Mh Boniface Tarakwa kumdhalilisha kwenye mkutano na hadhara kitongoji cha Ekenywa kwa kusema alitumia fedha za mradi wa maji shilingi milioni sitini jambo ambalo si ukweli.

Wakieleza hatua zilizofikia dhidi ya Mh Boniface Taraka pamoja na Mh Noah Lembris kuhusu maneno ya kashfa amesema kuwa Menyekiti ametiwa hatiani kwa kosa la kutoa maneno ya kashfa na ametoa neno lisilo na staha (MNAFIKI) na muongo na anapaswa kwenda kuombewa.

Hata hivyo kuhusu suala la mwenyekiti wa halmashauri kuema Mh Boniface Tarakwa ndiye anayezuia kata ya mwandeti isigawanywe  jambo lililojitokeza katika ziara ya mbunge wa Arumerukamati hiyo imeona hakukuwa na maeno ya uchochezi ala udhalilishaji kani lilikua ni ukumu lake katika kusimamia ugawaji a kata hiyo.

Wakitoa maamuzi mbele ya baraza la madiwani Kamati hiyo ya maadili kulingana na kanuni na tangazo la serikali kinalohusu madiwani namba 280 la tarehe 4 agosti 2000 wamesema kifungu cha 35 (c) kimetoa kimetoa adhabu ambazo zinaweza kutolewa kwa diwani ambaye ametiwa hatiani ka kuvunja kanuni za maadili a madiwani.

Wakielezea adhabu hizo wamesema diwani akitiwa hatiani anatakia kupewa kwa mara ya  kwanza na ya pili,Kumshitaki Diwani pamoja na kuweka taarifa za diwani huyo katika ripoti ya uajibikaji ya halmashauri nzima hivyo anatakiwa kupewa adhabu kwa mujibu wa kanuni hizo.

No comments