WATOTO WA KIKE WAASWA KUSOMA MASOMO YA SAYANSI NA HISABATI Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulukia Muungano na Mazingira January Makamba (kulia) akimsikiliza Msajili wa Bodi ya Wahandisi nchini Tanzania(ERB) Mhandisi Patrick Balozi (kushoto) akitoa neno la utangulizi wakati wa uzinduzi wa kongamano la tatu la wahandisi wanawake nchini mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulukia Muungano na Mazingira January Makamba (kulia) akimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Wahandisi Wanawake nchini Mhandisi Alice Isibike akielezea changamoto wanazokutana nazo wahandisi wanawake mapema hii leo wakati wa uzinduzi wa kongamano la tatu la wahandisi wanawake nchini mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulukia Muungano na Mazingira January Makamba akizungumza na wahandisi wanawake nchini wakati akizindua kongamano la tatu la wahandisi wanawake nchini mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wahandisi wanawake wakimsikiliza Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulukia Muungano na Mazingira January Makamba wakati akizindua kongamano la tatu la wahandisi wanawake nchini mapema hii leo jijini Dar es Salaam.Picha na Eliphace Marwa – Maelezo Na. Paschal Dotto- MAELEZO Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mhe. Janauary Makamba amewaasa watoto wa kike kusoma masomo ya sayansi ambayo yatawawezesha kupata utaalamu katika fani ya uhandisi. Akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Rais katika Tamasha la Wahandisi wanawake(TAWECE) lililofanyika katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salamu Mhe. Makamba amesema kuwa katika juhudi za kujenga taifa la viwanda fani ya uhandisi ni muhimu hivyo watoto wakike hawana budi kuweka kipaumbele katika masomo ya sayansi. “katika hali ya kawaida wahandisi wa kike ni wachache kulinganisha na wahandisi wa kiume hii ni kutoka na kuwepo kwa imani kuwa masomo katika kada hii ni ya wanaume na si wanawake kama watoto wengi wanavyojua,watoto wa kike onyesheni tofauti someni masomo ya sayansi muweze kutoa mchango kwa taifa “ Alisema Waziri Makamba. Pia Waziri Mhe. Makamba ameishukuru Serikali ya Norway kwa kutoa nafasi kwa masomo kwa watoto wa kike kusomea uhandisi kwani hali hii imesaidia kuongeza idadi ya wahandisi wa kike kutoka 96 kwa mwaka 2010 hadi kufikia wahandisi 379 kwa mwaka huu. Naye Mwenyekiti wa chama hicho Mhandisi Alice Sibike ameishauri Serikali ya Tanzania kuwawezesha watoto wa kike katika kuwapa fursa kwa kuwapa mikopo elimu ya juu ili kusaidia kuongeza idadi ya watoto wa kike wanaosoma fani uhandisi. Katika kutekeleza kwa vitendo mpango huo chama hicho kimeanza kutembelea shule mbalimbali na kutoa elimu kwa watoto wa kike kusoma masomo ya sayansi ambapo mpaka sasa wameshatembelea shule za Azania, Feza girls na Tambaza zote za jijini Dar es salaam. Mwenyekiti wa usajili wahandisi Mhandisi Patrick Balozi amesema ipo haja ya watoto wa kike na jamii kwa ujumla kuhamasika kuweka kipaumbele cha masomo ya sayansi kwa watoto wa ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuwa na uchumi wa viwanda. Tanzania ina jumla ya wahandisi 19,164 ambao kati yao wanawake ni 1,763 huku wahandisi 4831 wako mafunzoni baada ya kumaliza masomo na kati yao wa kike ni 372. “tunahitaji wahandisi 80000 ili kukidhi mahitaji ya kujenga nchi ya viwanda lakini watoke katika jinsia zote ili kuweka mfumo sawa katika kutenda kazi”, Alisema Mhandisi Balozi Tamasha la chama hicho lilianza rasmi mwaka 2015 na lengo ni kuwakutanisha wahandishi wote wa kike ili kubadilishana ujuzi na pia kuwawezesha watoto wa kike kujifunza kutoka kwa wahandisi wenye uzoefu Posted by MICHUZI BLOG at Friday, July 28, 2017 No comments: Links to this post Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest RAIS AAGIZA KUSIMAMISHWA KAZI KWA NAIBU KAMISHNA WA UHAMIAJI RAIS Dkt. John Magufuli amemuagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kumsimamisha kazi Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Bi. Grace Hokororo asimamishwe kazi kwa tuhuma za kuingiza nchini raia 50 wa Somalia na kuwapa vibali vya kuishi kinyume cha taratibu. Kauli hiyo imetolewa leo (Ijumaa, Julai 28, 2017), na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kumaliza kikao na Makamishna wa uhamiaji. Kikao hicho kilifanyika Makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam. Pia Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba kuunda tume ya uchunguzi kuhusu utoaji wa vibali uraia nchini. Amesema haiwezekani raia wa kigeni wanaingizwa nchini na wanapewa vibali vya kuishi bila ya kufanyiwa uchunguzi wa kina. “Idara ya Uhamiaji tunaitegemea kusimamia mipaka yetu na kuziba mianya ya watu kuingia bila ya kufuata taratibu lakini kwa mapenzi yake Ofisa huyu ameruhusu Wasomali kuingia bila kufuata taratibu.” Waziri Mkuu amesema ni lazima uchunguzi ufanyike ili kubaini “Tulidhani ni kitu gani kilimsukuma kutoa vibali kwa Wasomali hao ambao hawakuwepo nchini wameingia na kupewa vibali moja kwa moja kwa mapenzi yake tu sasa hii ni dosari hatuwezi kuivumilia.” Amesema Serikali inaitegemea Idara ya Uhamiaji kwa kuzuia mianya ya uingiaji raia mbalimbali kutoka nje ya nchi bila ya kufuata taratibu, hivyo Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli ameagiza Ofisa huyo asimamishwe kazi na uchunguzi ufanyike ili kubaini malengo yake. "Hawa Wasomali aliowapa vibali vya kuishi wala hawakuwa wanaishi nchini wameingia tu na kupewa vibali, hivyo Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli ameagiza ofisa huyo akae pembeni na achunguzwe ni kujua ni kitu gani kilimsukuma kutoa vibali kwa raia hao." Pia Waziri Mkuu ameiagiza idara ya Uhamiaji wadhibiti kitengo cha utoaji hati za kusafiria za Kibalozi na kwa wanaomaliza muda wasipewe tena. " Lazima hati hizo zikaguliwe katika mipaka yote na maeneo yote ya usafiri ili kujua kama huyo anayeitumia bado anahadhi hiyo na msiporidhika ichukuweni kwani kuna watu wanazitumia vibaya." Hata hivyo Waziri Mkuu ameagiza uchungilzi wa kina ufanyike kwa watu wote walioomba hati za kusafiria pamoja na vibali vya makazi kama wanakidhi matakwa ya kisheria kabla ya kuwakabidhi. IMETOLEWA NA: OFISI YA WAZIRI MKUU, IJUMAA, JULAI 28, 2017
Mgeni
Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulukia Muungano
na Mazingira January Makamba (kulia) akimsikiliza Msajili wa Bodi ya
Wahandisi nchini Tanzania(ERB) Mhandisi Patrick Balozi (kushoto) akitoa
neno la utangulizi wakati wa uzinduzi wa kongamano la tatu la wahandisi
wanawake nchini mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulukia Muungano na Mazingira January Makamba (kulia) akimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Wahandisi Wanawake nchini Mhandisi Alice Isibike akielezea changamoto wanazokutana nazo wahandisi wanawake mapema hii leo wakati wa uzinduzi wa kongamano la tatu la wahandisi wanawake nchini mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulukia Muungano na Mazingira January Makamba akizungumza na wahandisi wanawake nchini wakati akizindua kongamano la tatu la wahandisi wanawake nchini mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wahandisi wanawake wakimsikiliza Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulukia Muungano na Mazingira January Makamba wakati akizindua kongamano la tatu la wahandisi wanawake nchini mapema hii leo jijini Dar es Salaam.Picha na Eliphace Marwa – Maelezo
Na. Paschal Dotto- MAELEZO
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mhe. Janauary Makamba amewaasa watoto wa kike kusoma masomo ya sayansi ambayo yatawawezesha kupata utaalamu katika fani ya uhandisi.
Akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Rais katika Tamasha la Wahandisi wanawake(TAWECE) lililofanyika katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salamu Mhe. Makamba amesema kuwa katika juhudi za kujenga taifa la viwanda fani ya uhandisi ni muhimu hivyo watoto wakike hawana budi kuweka kipaumbele katika masomo ya sayansi.
“katika hali ya kawaida wahandisi wa kike ni wachache kulinganisha na wahandisi wa kiume hii ni kutoka na kuwepo kwa imani kuwa masomo katika kada hii ni ya wanaume na si wanawake kama watoto wengi wanavyojua,watoto wa kike onyesheni tofauti someni masomo ya sayansi muweze kutoa mchango kwa taifa “ Alisema Waziri Makamba.
Pia Waziri Mhe. Makamba ameishukuru Serikali ya Norway kwa kutoa nafasi kwa masomo kwa watoto wa kike kusomea uhandisi kwani hali hii imesaidia kuongeza idadi ya wahandisi wa kike kutoka 96 kwa mwaka 2010 hadi kufikia wahandisi 379 kwa mwaka huu.
Naye Mwenyekiti wa chama hicho Mhandisi Alice Sibike ameishauri Serikali ya Tanzania kuwawezesha watoto wa kike katika kuwapa fursa kwa kuwapa mikopo elimu ya juu ili kusaidia kuongeza idadi ya watoto wa kike wanaosoma fani uhandisi.
Katika kutekeleza kwa vitendo mpango huo chama hicho kimeanza kutembelea shule mbalimbali na kutoa elimu kwa watoto wa kike kusoma masomo ya sayansi ambapo mpaka sasa wameshatembelea shule za Azania, Feza girls na Tambaza zote za jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa usajili wahandisi Mhandisi Patrick Balozi amesema ipo haja ya watoto wa kike na jamii kwa ujumla kuhamasika kuweka kipaumbele cha masomo ya sayansi kwa watoto wa ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuwa na uchumi wa viwanda.
Tanzania ina jumla ya wahandisi 19,164 ambao kati yao wanawake ni 1,763 huku wahandisi 4831 wako mafunzoni baada ya kumaliza masomo na kati yao wa kike ni 372.
“tunahitaji wahandisi 80000 ili kukidhi mahitaji ya kujenga nchi ya viwanda lakini watoke katika jinsia zote ili kuweka mfumo sawa katika kutenda kazi”, Alisema Mhandisi Balozi
Tamasha la chama hicho lilianza rasmi mwaka 2015 na lengo ni kuwakutanisha wahandishi wote wa kike ili kubadilishana ujuzi na pia kuwawezesha watoto wa kike kujifunza kutoka kwa wahandisi wenye uzoefu

No comments