HATIMAYE HAMISA MOBETO AANIKA KILA KITU,AFUNGUKA HAYA MAZITO KWENYE MAHOJIANO LIVE
Tangu
ilipoachiwa video ya ‘Salome’ ya mkali wa Bongofleva Diamond Platumz
akishirikiana na Rayvanny, kulianza maneno kuwa Diamond anatoka
kimapenzi na mwanamitindo Hamisa Mobeto.Hamisa alikuwa mmoja wa warembo
walioonekana kwenye video hiyo.
Wiki kadhaa mbele, Hamisa alionekana
kuwa na ujauzito na hapo ndipo maneno yalipozidi kwenda mbali zaidi
kwamba mhusika wa mimba hiyo ni mwanamuziki Diamond.
Yafuatayo
ni mazungumzo kati ya muandishi wa habari na bibie Hamisa Mobeto kuhusu
suala hilo:
Hamisa alisema kuwa ni kweli amesekia maneno mengi kuhusu
mimba yake akihusishwa mwanamuziki Diamond kama inavyosemwa.
“Huu
uvumi unataka niweke wazi maisha yangu. Hilo halitajitokeza kwangu
kwani mtu akishaumwa na nyoka akimuona mjusi anamuogopa. Baba wa mtoto
wangu mtarajiwa namjua mimi na familia yangu. Nadhani inatosha.
“Sidhani
kama ni lazima nimtaje kwenye media (vyombo vya habari) lakini wale
wanaosema ni Diamond tafadhali sana, siye. Baba wa mtoto wangu yupo na
sio matangazo ya biashara kila mtu majue mpenzi wangu.
“Hao
wanaotutukana mbona maisha yao wameyaweka siri, au mimi tu ndiyo
nijianike? Siwezi kufanya hivyo, najua nachokonolewa ili niseme lakini
sitasema,” amesema Hamisa.
Amesema
kuwa kwa sasa yeye ni mtu mpya na kwamba mashabiki wake watamjua kwa
kazi zake na siyo maisha yake binafsi kwa sababu ameshajua madhara ya
maisha yake hadharani.
“Maisha
yangu binafsi yatabaki kuwa yangu mimi mwenyewe ila ya kibiashara
yatajulikana na kila mtu. Mimi kwa sasa sihitaji sifa za kijinga,
nahitaji mashabiki zangu wafahamu nafanya nini katika jamii na
wanishabikie hivyo, sio kwa maisha yangu binafsi,” amesema.
“Kuruhusu
ushabiki katika maisha yako binafsi hasa ya mapenzi ni kujijengea uadui
na marafiki wa uongo ambao wengi wao wanakuja kinafiki na kujifanya
wanakufahamu kiundani au mpenzi wako kumbe ni waongo. Wanataka
kuwavuruga na wakifanikiwa hutawaona,” alisema.

No comments