Simba apatikana akimnyonyesha mwana wa Chui Tanzania
Mwana wa chui hawezi kubadili madoa doa katika ngozi yake lakini simba huyo hajali hilo.
Picha
hizi ni za kwanza kuchukuliwa simba akimnyonyesha mwana wa chui kutoka
jamii nyengine ya wanayama, kisa kisicho cha kawaida.
Wawili hao
walionekana na Joop Van Der Linde mgeni katika katika eneo la Ndutu
safari Lodge nchini Tanzania katika eneo la uhifadhi la wanyma pori la
Ngorongoro.

Eneo hilo ni la Serengeti. Simba huyo amepewa jina Nosikitok na ana umri wa miaka mitano.
Simba
huyo amewekewa mfumo wa GPS katika shingo yake ili kutambua anakokwenda
na ana watoto watatu waliozaliwa kati ya mwezi Juni 27-28.

Daktari Luke Hunter , ambaye ni rais muhifadhi mkuu
wa Panthera ,shirika kuu la ufugaji wa wanyama aina ya paka aliambia BBC
kwamba kisa hicho ni cha kipekee.

Sio kitu ambacho nilijuwa ambapo simba angeweza kuwalea watoto wa simba mwengine.,...hiki ni kisa tofauti sana.
Sina
kisa chengine chochote nikijuacho kati ya familia ya mnyama paka kwa
mfano pale ambapo mnyama mmoja amechukua mwana wa mnyama mwengine katika
familia hiyo hiyo na kumnyonyesha.
Simba wengi wa kike huwauwa watoto wa chui wanapokutana nao, na huwaona kama wapinzani katika mapambano ya kutafuta chakula.
Daktari
Hunter anasema Nosikitok ana watoto wachanga walio na umri sawa na
mwana huyo wa chui wakiwa na wiki mbili hadi tatu hivi.

Simba huyo alikuwa kilomita moja kutoka kwa nyumba yao ambapo kuna maficho ya watoto wake alipokutana na chuo huyo mdogo.
Alimchukua mwana huyo na kumlea kama wake na humlindi dhidi ya shambulio lolote

No comments