Balozi Mwapachu ajitoa katika Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Acacia
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni ya uchimbaji ya Acacia, Balozi Juma Mwapachu amestaafu nafasi hiyo baada ya kuitumikia kwa vipindi viwili.
Mwapachu
amechukua uamuzi huo leo, Julai 13 baada ya muhula wake wa pili wa
miaka mitatu mitatu wa ujumbe wa bodi hiyo, kumalizika.
Taarifa
iliyotumwa leo na Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya Acacia imeeleza
kuwa inamshukuru Balozi Mwapachu kwa utendaji wake na ushirikiano wake
wote alipokuwa mjumbe.
“Tunamtakia maisha mema,” imesema taarifa hiyo.
Kutokana na mabadiliko hayo, Bodi ya Acacia itabaki na wajumbe saba, wakiwamo wanne wakurugenzi na wasio wakurugenzi.

No comments