Dr. Mengi ataka wasambazaji kushawishi uwekezaji
Meneja Mkakati wa Kampuni ya Agricom Afrika, Eric Mwidunda (kushoto)
akitoa maelezo kuhusu ubora wa matrekta hayo kwa Mwenyekiti wa Taasisi
ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi (wa pili kushoto)
alipotembelea kwenye Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa
yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere
(Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam
Makampuni
ya Tanzania ya uwakala wa usambazaji wa bidhaa za kutoka nje ya nchi,
wameshauriwa kuyashawishi makampuni ya nje kujenga viwanda vya kuzalisha
bidhaa hapa hapa nchini.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi
ametoa ushauri huo jijini Dar es salaam wakati akitembelea mabanda ya
maonyesho ya Kimataifa ya Biashara, na kusisitiza kuwa kwa kufanya hivyo
watakuwa wanaunga mkono kwa vitendo jitihada za Rais John Pombe
Magufuli za kutaka kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald
Mengi akielekea kukagua baadhi ya matrekta katika banda la Kampuni ya
Agricom akiambatana na Meneja Mkakati wa Kampuni ya Agricom Afrika, Eric
Mwidunda (kulia kwa Dr.Mengi) alipotembelea kwenye maonesho ya 41 ya
Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho ya
Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es
Salaam.
Akifuatana na Mkurugenzi wa TPSF Bw. Louis Accaro, Afisa Biashara wa
Tan-Trade Bw. Mohamed Mkadara, na Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake
Wajasiriamali Bi. Jacquiline Maleko, Dr Mengi ametembelea mabanda
mbalimbali, yakiwemo yaliyopo chini ya mwamvuli wa Chama cha
wafanyabiashara wenye viwanda, na Kilimo – TCCIA, Mfuko wa Fursa sawa
kwa wote-EOTF, na Banda la Kampuni ya Agricom, ambayo Mkurugenzi wake
Mtendaji Bi. Angelina Ngalula alielezea jinsi ilivyojipanga kusambaza
zana za kisasa za kilimo ili kumpunguzia mkulima gharama za uzalishaji.
Katika majumuisho yake Dr Mengi alishauri Tan-Trade na TPSF washirikiane
katika kuangalia namna ya kuboresha zaidi maonyesho hayo, hususan
katika kuboresha mabanda ya maonyesho ili yalingane na hadhi halisi ya
kimataifa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Agricom, Bi. Angelina Ngalula
(kushoto) akikabidhi zawadi kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi
Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi alipotembelea banda la kampuni hiyo
kujionea huduma zao kwenye Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa
yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere
(Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa miradi na mshauri wa Maisha Finance Ltd, ambao ni
wakopeshaji wa zana zote za kilimo yakiwemo Matrekta ya kampuni ya
Agricom, Erasmus Erneus akitoa ufafanuzi kwa mmoja wa wateja, Apollos
Rweikiza aliyetembelea banda la Agricom katika Maonesho ya 41 ya
Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Uwanja wa maonesho ya
Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es
Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald
Mengi akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa Chama Cha Wanawake
Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) Jacqueline Maleko (wa pili kushoto)
alipowasili kwenye banda la TWCC yanakoendelea maonesho ya 41 ya
Biashara ya Kimataifa katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K
Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Fedha, Masoko na Usafirishaji wa C.E Holdings Ltd,
wauzaji wa vito vya Afrika, Maria Pagama akitoa maelezo kwa Mwenyekiti
wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi
alipotembelea banda la TWCC kwenye maonesho ya 41 ya Biashara ya
Kimataifa yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K
Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Picha juu na chini ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania –
TPSF Dr Reginald Mengi akifurahia jambo na wanawake wafanyabiashara
kwenye banda la TWCC katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa
yanayoendelea Uwanja wa maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba
Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Picha ya juu kulia ni
Noreed Mawalla wa Chama Cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC).

Mkurugenzi wa Tanfood and Spice Co. Investment watengenezaji wa bidhaa
za kutunza ngozi zinazotokana na mimea, Bi. Rona akitoa maelezo ya
bidhaa halisi za kutunza ngozi kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta
Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi alipotembelea banda la TWCC
kwenye maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika
Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara
ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald
Mengi akitoa maelekezo kwa Noreed Mawalla wa TWCC (katikati) wakati
akitembelea banda la Chama cha wafanyabiashara wanawake kwenye maonesho
ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea viwanja vya maonesho ya
Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Wanawake Wafanyabiashara
Tanzania (TWCC) Jacqueline Maleko.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald
Mengi akitazama bidhaa mbalimbali katika banda la Chama Cha Wanawake
Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) lililopo katika maonesho ya 41 ya
Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa
akimuongoza Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr.
Reginald Mengi mara baada ya kuwasili katika banda la EOTF kwenye
maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es
Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald
Mengi akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Joane Art Craft,
Culture & Desigin, Bi. Joane Baigana (kulia) alipotembelea banda la
EOTF kwenye maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika
Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara
ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald
Mengi akitazama kazi mbalimbali za wakinamama wajasiriamali kwenye banda
la EOTF katika maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea
Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara
ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa
Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald
Mengi akisalimiana na wanawake wajasiriamali wanaofadhiliwa na EOTF
akiendelea kutembelea wajasiriamali katika maonesho ya 41 ya Biashara ya
Kimataifa yanayoendelea kwenye Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl
J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Anayemuongoza ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama
Anna Mkapa.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald
Mengi akisaini kitabu cha wageni katika banda la Kituo cha Sheria na
Haki za Binadamu lililopo ndani ya banda la EOTF yanakoendelea maonesho
ya 41 ya Biashara ya Kimataifa katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa
Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald
Mengi akitazama moja ya vitabu katika banda la Kituo cha Sheria na Haki
za Binadamu lililopo ndani ya banda la EOTF. Kulia kwake ni Mwenyekiti
wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald
Mengi akipata maelezo ya huduma mbalimbali za mikopo riba nafuu kwa
wanawake kutoka kwa Afisa Huduma kwa Wateja wa Tanzania Women's Bank,
Renita Michael (kulia) ndani banda la EOTF wakati alipotembelea maonesho
ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Uwanja wa maonesho
ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar
es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote
(EOTF), Mama Anna Mkapa na Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Wanawake
Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) Jacqueline Maleko.
No comments