Zuma matatani tena
Rais wa Afrika
kusini Jacob Zuma anachunguzwa tena baada ya kuvuja kwa idadi kubwa ya
barua pepe, zinazodai kugundua mtandao wa rushwa kati yake na familia ya
Guptas yenye ushawishi kibiashara.
Nyaraka hizo zinadai kwamba Gupta wangepata dola laki saba na nusu.
Hata hivyo familia ya Gupta bado hawajazungumza chochote kuhusiana na shutuma hizo.
Picha
GALLO IMAGES Mtoto wa Rais Zuma (kulia).Msemaji wa Rais Zuma amepinga taarifa hizo na kusema kuwa ni za kutengenezwa.

No comments