TASAF YAPUNGUZA HALI YA UTAPIAMLO


Wanakijiji wamiwa wamefurahi baada ya kuwaona wageni wamewatembelea katika kijiji Sing'isi mara tu ya kuwasili katika eneo hilo kama wanavyoonekana katika picha.Picha na Vero Ignatus Blog
 Wanakijiji cha Sing'isi  wakiwa wageni.Picha na Vero Ignatus Blog
Wanakijiji wa Sing'isi wakiwa wanawasikiliza wageni kutoka TASAF walipowatembelea kijijini hapoi.Picha na Vero Ignatus Blog

Na .Vero Ignatus Arusha.

Mradi wa kunusuru kaya masikini waf katika kijiji cha Singisi wilaya ya Meru umesaidia kupunguza hali ya utapiamlo kwawatoto na wazazi kutokana na wananchi wanaonufaika kutumia fedha hizo katika kilimo cha umwagiliaji hali inayowahakikishia upatikanaji wa chakula katika kaya zao.
Wananchi wa Kijiji hicho wamesema kuwa kufuatia hali ngumu za uchumi zilizokua zikiwakabili walishindwa kupata milo mitatu katika kaya zao lakini kwa sasa wanalima na wanafuga kuku na kupata mayai ambayo hutumia katika kuboresha mlo wao

Mwakilishi wa Tasaf kutoka Makao makuu Msangi Sitonga amesema kuwa miradi hiyo imewasaidia wananchi kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini uliokithiri hivyo amewataka wananchi kutumia fedha hizo kwa manufaa yaliyokusudiwa ili kutimiza lengo la mradi huo

Mwezeshaji wa Tassaf Wilaya ya Meru Boniface Mwilenga akitoa taarifa ya mradi huo amesema kuwa jumla ya watu  159  wamenufaika na mradi huo ambao umegusa zaidi ya kaya ambazo kwa sasa zimeondokana na umasikini ulikithiri
 

No comments