MSIUZE hOVYO CHAKULA KABLA YA KUWA NA AKIBA YA KUTOSHA- RC TABORA
Na Tiganya Vincent-RS-Tabora
Wakazi
wa Mkoa wa Tabora wametakiwa kuweka akiba ya chakula cha kutosha ili
kuepuka njaa inayoweza kuwakabili kutokana na mavuno ya msimu huu
kutokuwa mazingira kufuatia mvua kuchelewa kuanza na kuwahi kukatika.
Wito
huo umetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri wakati wa
kilele cha maadhimisho siku ya mazingira duniani ambapo kimkoa
yalifanyika katika Manispaa ya Tabora.
Alisema
mvua za msimu huu zilikuwa kidogo na hivyo mavuno ya mazao kama vile
mahindi , mpunga na maharagwe ni hayaridhishi hivyo ni vema wananchi
wakahakikisha wanatenga chakula cha kutosha kwa ajili ya matumizi yao
kabla ya kuanza kuuza.
Mkuu
huyo Mkoa alisema kuwa kuna baadhi ya wafanyabiashara kutoka Mikoa
mbalimbali wamekuwa wakipita katika maeneo mbalimbali ya vijiji na
kuwarubuni wakulima wawauzie mahindi yao nao bila kuchukua tahadhari
wanafanya wamekuwa wakiuza bila kuweka akiba ya kutosha jambo ambao sio
jema.
Aliongeza
kuwa watu aina hiyo ambao wanakimbilia kuuza mahindi yao bila kuweka
aakiba ya kutosha kwa ajili ya familia zao ndio wamekuwa wakimbilia kwa
viongozi wa Serikali wanaishiwa chakula.
Mkuu
huyo wa Mkoa alisisitiza kuwa ameamua kuwatahadharisha mapema ili kila
mkazi wa Tabora akatumia fursa hii ya upatikanaji wa vyakula vya kutosha
katika masoko kuweka akiba kwa ajili ya familia zao badala ya kukaa ili
kugonja msaada na wakati mwingine kulaumu Serikali bila sababu za
msingi.
“Nawaombeni
tunzeni chakula mlichokipata kwa ajili ya matumizi ya baadaye badala
kukimbilia kuuza na kutengenezea pombe za kiinyeji…jambo hili ni hatari
kwa kuwa unapokosa chakula unageuka mtumwa na wakati mwingine unaweza
hata kudhalilishwa na mtu mwenye chakula” aliwatahadharisha wakazi wa
Tabora
Aidha
Bw. Mwanri aliwaagiza Wakuu wa Wilaya zote kuhakikisha wanasimamia
zoezi la kufanya tathimini ya chakula kilichopo katika maeneo yao na
kuhakikisha hakuna uuzaji wa holela holela wa mahindi ili kuchukua
tahadhari ya kukabiliana na tishio upungufu wa chakula kwa wakazi wa
Tabora.
Alisema kuwa mtu asiuze chakula kama hana akiba inayoweze kumfikisha mkulima katika mavuno ya msimu ujao.
Bw.
Mwanri alisisitiza kuwa Wakuu hao wa Wilaya wahakikishe viongozi wote wa
Serikali za Vijiji na Mitaa wanasimamia zoezi la kuhakikisha kuwa mtu
anayeuza mahindi anayo akiba ya kutosha na sio vinginevyo ili kuepuka
tabia ya watu kukimbilia kuuza mahindi hivi sasa wakiishiwa wanaanza
kukimbilia kwa viongozi.

No comments