Raisi Magufuli: Hata mkeo anaweza asikupende siku nyingine, cha muhimu ni kuchapa kazi
Rais
Magufuli leo mkoani Mtwara wakati akiweka jiwe la msingi katika kituo
cha kupooza umeme njia ya KV 132 amelipongeza Shirika la Umeme nchini
Tanesco na kumpongeza Waziri wa Nishati na Madini, kwa juhudi zake
katika kazi.
Rais
Magufuli amesema aliamua kumteua Sospeter Muhongo kuwa Waziri kutokana
na ukweli kwamba alikuwa anaona uchapaji wake wa kazi kipindi ambacho
yeye ni Waziri wa Ujenzi.
"Lengo
lililokuwa kwenye ilani ya Uchaguzi kwa mwaka jana ilikuwa asilimia
thelathini na kitu nyinyi mkafika mpka asilimia arobaini, na sasa hivi
mko zaidi ya asilimia 46 sasa nisipowapongeza nitakuwa mtu mbaya wa moyo
mbaya.
" Na mimi na moyo mzuri kweli ndiyo maana nawapongeza wizara pamoja na Tanesco haya matatizo mengine ambayo yanatokea ni kwa sababu tuliingia mikataba ya hovyo huko nyuma, ya kulipia capacity charges ninajua mnayashughulikia na tunajaribu kutafuta pesa za mikopo tulipe haya madeni twende na Tanesco mpya" alisema Rais Magufuli

Mbali na hilo Rais Magufuli alimsihi Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo
"Nilipoteuliwa
kuwa Rais sikuona mtu mwingine anayefaa kama Muhongo, nikamrudisha hapa
hapa sababu mimi nilipokuwa nikihesabu kilometa za barabara yeye
alikuwa anaesabu kilometa za nyaya, kwa hiyo nilifahamu kazi yake na saa
zingine ukifanya kazi vizuri unakuwa kama hupendwi pendwi hivi, lakini
kwa nini wakupende? Hata mke wako anaweza asikupende siku zingine, wewe
chapa kazi" alisisitiza Rais Magufuli
Rais Magufuli aliendelea kusisitiza kuwa katika maisha ya kila siku huwezi kupendwa na kila mtu
"Hata
ndugu yako anaweza asikupende, saa zingine hata baba yako au hata mdogo
wako anaweza asikupende, huwezi ukapendwa na kila mmoja, hata mitume
hawakupendwa na wote na wengine walisulubiwa pamoja na kwamba walifanya
mazuri.
"Kwa hiyo Prof. Muhongo wewe fanyakazi tena usihangaike hata kusoma ile mitandao, mimi sisomagi hiyo mitandao achana nayo watandae huko huko wenyewe wewe chapa kazi" alisisitiza Mhe. Rais Magufuli.
"Kwa hiyo Prof. Muhongo wewe fanyakazi tena usihangaike hata kusoma ile mitandao, mimi sisomagi hiyo mitandao achana nayo watandae huko huko wenyewe wewe chapa kazi" alisisitiza Mhe. Rais Magufuli.

No comments