Operesheni ya Viroba Yaibua Wafanyabiashara Wasiokuwa na Vibali vya TFDA.
Na: Lilian Lundo – MAELEZO.
Operesheni
ya kuondoa pombe kali zilizofungwa katika vifungashio vya plastiki
(viroba) inayoendelea nchi nzima imeibua wafanyabiashara wanaofanya
biashara ya pombe bila kuwa na vibali vya Mamlaka ya Chakula na Dawa
(TFDA).
Hayo
yamebainishwa na Afisa Afya na Mratibu wa Masuala ya Chakula wa Manispaa
ya Temeke Rehema Sadick, leo Jijini Dar es Salaam wakati wa operesheni
hiyo inayoendelea nchini.
“Katika
operesheni hii ya kuondoa pombe za viroba tumegundua wafanyabiashara
wengi wanaojihusisha na uuzaji wa pombe kutokuwa na kibali cha TFDA
ambacho hutolewa katika Halmashauri husika,” alifafanua Rehema Sadick.
Aidha
amebainisha kuwa katika msako uliofanyika leo Kigamboni, ambapo
wamekagua zaidi ya maduka matano yanayouza pombe kwa jumla, ni duka moja
tu la Mangale Store lililoko Tuangoma ndilo lililokutwa na kibali cha
TFDA.
Aliongeza
kuwa, maduka yote ambayo hayakuwa na vibali hivyo yameamuliwa kufungwa
na kufuatilia vibali katika Halmashauri husika na taarifa za maduka hayo
ikiwemo jina la duka, majina ya mmiliki eneo lilipo pamoja na namba za
mawasiliano vimechukuliwa kwa ajili ya kuchukua hatua.
Afisa
Afya huyo ametoa rai kwa wafanyabiashara wote kuacha kufanya biashara
kwa mazoea na kuhakikisha wanakuwa na vibali vyote muhimu pamoja na
leseni za biashara, kwani kutofanya hivyo ni kukiuka sheria na kanuni za
nchi.
Operesheni
ya kuondoa viroba ilianza rasmi Machi 01, 2017 kufuatia agizo la Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa la kutaka kusitishwa kwa utengenezaji, usambaaji,
uuzaji na utumiaji wa pombe hizo kali maarufu kama viroba.ifikapo Machi
mosi mwaka huu ambapo mpaka sasa operesheni hiyo imeingia siku ya tano
tangua kuanza kwake.

No comments