MBUNGE WA KIBAHA MJINI KOKA AHIDI KULITATUA TATIZO LA MAJI KWA WAKAZI WA KATA YA PANGANI
WAKINAMAMA wa kata ya Pangani wanaoishi katika mitaa minne ya Lumumba,Kidimu, Liwale pamoja ma mkombozi katika halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mji Mkoa wa Pwani wanakabiliwa na kero kubwa ya ukosefu wa maji safi na salama hivyo kuwalazimu wakati mwingine kuamka usiku wa manane kwa ajili ya kwenda kuchota maji visimani kitu ambacho kinahatarisha usalama wa maisha yao kutokana na mazingira yenyewe kuwepo katika mapori.
Kilio
hicho cha wakinamama hao wamekitoa baada ya Mbunge wa Jimbo la Kibaha
mjini Silvestry Koka kufanya ziara yake ya kikazi katika mitaa mbali
mbali iliyopo katika kata ya Pangani kwa lengo ya kuweza kufanya ukaguzi
wa miradi ya maendeleo na kuweza kuzungumza na wananchi ili kubaini
changamoto ambazo zinawakabili.
Wakinamama
hao akiwemo Maria Benjamini ,Zawadi Ibrahimu,pamoja na Asimu Mendani
walisema kuwa wanashindwa kufanya shuguli nyingine za kuleta maendeleo
kutokana na kutumia muda mwingi wa kutafuta maji hivyo wameiomba
serikali kupitia mamlaka zinazohusika kuliingilia kati suala hilo kwa
lengo la kuweza kuwapatia huduma ya maji.
Kilio
cha wakinamama hao kinamgusa na kumwinua Mbunge wa Jimbo la Kibaha
mjini Silvestry Koka na kuamua kumwagiza mbele ya mkutano wa adhara
Injinia wa maji katika halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mji kuhakikisha
wananchi wa mitaa minne ya Kidimu, Lumumba,miwale pamoja na mkombozi
iliyopo kata ya Pnagani wanapata maji ya bomba haraka ili waweze
waondokana na adha waliyokuwa wanakabiliana nayo kwa muda mrefu.
Koka
alisema kwamba suala hilo hawezi kulifumbia macho hata kidogo na
atahakikisha kwamba analivalia njuga kwa lengo la kuweza kuona wananchi
wake wa kata ya Pangani wanapata maji safi na salama na kuondokana na
adha ambayo wamekuwa wakiipata kwa kipindi cha muda mrefu.
“Ndugu
zangu wananchi wa kidimu ninachotaka kusema ni kwamba ninamwagiza
Injinia wa maji kuhakikisha kwamba katika mitaa yote minne maji
yanapatikana ili wananchi waweze kuondokana na usumbufu huu hususan
wakinamama wanaamka nyakati za usiku kwenda kutafuta maji kitu ambacho
mimi kama Mbune wenu sitaki kukiona ninachotaka ni maji,”alisema Koka.
Akijibu
malalamiko yaliyotolewa na wananchi hao wa pangani Mbele ya Mbunge
kuhusina na kilio chao cha siku nyingini juu ya kero sugu ya upatikanaji
wa maji Injinia wa halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mjini Grace Limo
amesema kuwa kwa sasa taratibu zote zimeshafanyika la kuweka bomba kubwa
ambalo litakiuwa likisambaza maji katika maeneo mbali mbali ya Kibaha
kutoka mtambo wa Ruvu juu.
KUWEPO
kwa tatizo sugu la upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi wa
kata ya Pangani katika halmashauri ya Wilaya ya Mji wa Kibaha
kusababisha baadhi ya wakinamama kuacha familia zao wakiwemo watoto
watogo nyakati za usiku kwa ajili ya kwenda kuchota maji hivyo
kunahitajika juhudi za makusudi kutoka serikali katika kulitafutia
ufumbuzi wa kudumu suala hilo.
Mbunge
wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka akizungumza na wananchi wa kata
ya Pangani baada ya kufanya ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kuweza
kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi
kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili.
Mbunge
wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka akiwawahutubia wananchi wa kata
ya pangani katika mkutano wa adhara baada ya kufanya ziara yake ya
kikazi kwa ajili ya kukagua miradi ya maendeeo.
Baadhi
ya wananchi wa kata ya pangani katika halmashauri ya Wilaya ya Kibaha
mji wakimsikiliza Mbunge wakati akiwahutubia katika mkutano wa adhara
uliofanyika katika viwanja vya mtaa wa kidimu.
Diwani
wa kata ya Pangani Agustino Mdachi akifafanua jambo kwa wananchi katika
mkutano huo uliondaliwa na mbunge ikiwa ni moja ya ziara yake ya
kikazi.(NA VICTOR MASANGU, KIBAHA )
No comments