MAHAKAMA YA KISUTU KUFANYA UTAFITI WA KINA KABLA YA KUTOA MAAMUZI DHIDI YA KESI MPYA YA MKE WA MAREHEMU ERASTO MSUYA
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema inahitaji kufanya utafiti wa kina kabla
ya kutoa maamuzi dhidi ya kesi mpya inayomkabili mke wa marehemu
bilionea Erasto Msuya, Mariam Mrita (41) na mfanyabiashara Revocatus
Muyela (40).
Hakimu
Mkazi Thomas Simba amesema hayo Leo asubuhi wakati kesi hiyo ya mauaji
ilipofika mahakamani hapo kwa ajili ya kutolewa amuzi wa ifutwe au la
kutokana na mabishano ya upande wa serikali na ule wa utetezi.
Washtakiwa
Mrita na mwenzake Muyela waliachiwa huru mapema mwezi uliopita na kisha
wakakamatwa tena na kusomewa upya Mashtaka ya mauaji.
Katika kesi hiyo, Washtakiwa hao wanatuhumiwa kumuua kwa makusudi Aneth Msuya ambaye ni Dada wa bilionea Erasto Msuya.
Mauaji hayo yanadaiwa kutendeka huko Kibada Kigamboni Jijini Dar es Salaam.,Mei 25, mwaka jana.
Akiahirisha kesi hiyo, Hakimu Simba amesema Kuwa bado anafanya utafiti juu ya kesi hiyo."Maombi
yaliyoletwa na upande wa utetezi na mjibu ya Jamuhuri, yanahitaji
kifanyiwa utafiti wa kina kaba sijatoa uamuzi" amesema Hakimu Simba.
Kutokana na hayo, kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 20 kwa ajili ya kutolewa Manji.
Awali
mara baada washtakiwa kusomewa tuhuma zao za, mauaji, Wakili wa
washtakiwa, Peter Kibatala aliiomba Mahakama kufuta kesi hiyo akidai
kuwa kuwa imefunguliwa kinyume na sheria kwani ilishafutwa.
Alidai
kuwa kesi hiyo imefunguliwa kinyume na sheria kwa sababu ilishatolewa
uamuzi Februari 23, mwaka huu mbele ya Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambapa
ambapo aliwaachia huru washitakiwa wote.
"Maneno
aliyoyatumia Hakimu katika uamuzi wake ni amewa-set free washitakiwa na
si kuwa-discharge, hivyo hawa washitakiwa wapo huru na hawakupaswa
kukamatwa na kuletwa mahakamani kusomewa kosa hilo la mauaji," alidai
Kibatala.
Aidha
alidai kuwa Mahakama hiyo haikuwa na mamlaka ya kulipokea jalada hilo
na kuwasomea washitakiwa mashtaka yao kwa kuwa limeshatolewa uamuzi.
Akijibu hoja hizo Wakili wa Serikali Mutalemwa Kishenyi amedai kuwa washitakiwa wamesomewa kosa hilo kwa mujibu wa sheria.
Amedai
kuwa uamuzi uliotolewa ulikuwa ni kuwafutia mashitaka ambapo Jamhuri
ina uwezo wa kuwakamata tena washitakiwa na kuwasomea kosa hilo la
mauaji.
Amebainisha kuwa haoni sehemu yeyote ambayo inaonesha kosa walilosomewa washitakiwa lipo kimakosa mahakamani hapo
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

No comments