CHUO CHA MIPANGO- DODOMA CHAHIMIZA MATUMIZI YA TAFITI KUKABILIANA NA ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIA NCHI
Wajumbe
wa mkutano wa Mabadiliko ya tabia ya nchi na athari zake kiuchumi hapa
nchini uliokishirikisha Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini –Dodoma
na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU), wakiingia kwenye ukumbi wa Mikutano
mmoja Jijini Dar es salaam, siku ya kwanza ya mkutano huo wa Siku mbili.
Mwenyekiti
wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo vijijini –
Dodoma, Prof. Razack Lokina (kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano
uliohusu changamoto za mabadiliko ya tabia ya nchi wakati wa mkutano
uliowashirikisha wadau wa maendeleo kutoka ndani nan je ya nchi na
kuandaliwa na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini-Dodoma.
Mmoja
wa washiriki wa mkutano huo akichangia mada mbalimbali kuhusu
mabadiliko ya tabia ya nchi yanavyoathiri uchumi wa wananchi vijijini
nchini Tanzania, zilizowasilishwa kwenye mkutano ulioandaliwa na Chuo
cha Mipango ya Maendeleo Vijijini-Dodoma, na kufanyika Jijini Dar es
salaam.
Baadhi
ya wadau wa mkutano uliohusu changamoto za athari za uharibifu wa
mazingira na mabadiliko ya tabia ya nchi wakifuatilia kwa makini mjadala
kuhusu suala hilo, Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo vijijini –
Dodoma, Prof. Razack Lokina (kushoto) na Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Frank
Hawassi (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja nje ya ukumbi wa mkutano
kuhusu Mabadiliko ya Tania Nchi uliowashirikisha wadau kutoka ndani na
nje ya nchi uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo vijijini – Dodoma Dkt. Frank Hawassi
akizungumza na wajumbe wa Taasisi na Washirika wa Maendeleo kuhusu,
umuhimu wa kuunganisha nguvu katika kupambana na mabadiliko ya Tabia
nchi, katika Mkutano wa Mabadiliko ya Tabia nchi jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti
wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo vijijini –
Dodoma, Prof. Razack Lokina akizungumza na wadau na Washirika wa
Maendeleo kuhusu mradi wa Chololo Ecovillage uliopo Dodoma unaofadhiliwa
na Umoja wa Ulaya (EU) wakati wa Mkutano wa Mabadiliko ya Tabia nchi
jijini Dar es salaam.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM).
Na Benny Mwaipaja,WFM
Wadau
wanaofanya tafiti mbalimbali za Maendeleo ya uchumi nchini hasa maeneo
ya vijijini kuhusu Mabadiliko ya Tabia nchi wametakiwa kuwasilisha
matokeo ya tafiti hizo Serikalini na katika Mashirika mengine ya
Maendeleo ili matokeo yake yafanyiwe kazi na kusudio la tafiti hizo
liweze kufikiwa.
Rai
hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi
wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo vijijini – Dodoma, Prof. Razack Lokina
wakati wa Mkutano uliohusu mabadiliko ya tabia nchi na athari zake
kiuchumi uliozihusisha Taasisi za Serikali na Binafsi pamoja na
Washirika wa Maendeleo.
Amesema
Chuo cha Mipango kimekuwa kikifanya kazi zake vijijini, zikiwemo za
tafiti mbalimbali na matokeo hayo huwasilishwa katika ngazi husika
ikiwemo Ofisi ya Makamu wa Rais inayoshughulikia mazingira pamoja na
Wizara ya Maliasili na Utalii ili kutumia matokeo hayo kwa manufaa ya
maendeleo ya jamii hasa vijijini.
“Mkutano
wa Mabadiliko ya Tabia nchi ambao umejadili mbinu mbalimbali za
kukabiliana na athari za kiuchumi zinazotokana na Mabadiliko hayo,
umetokana na andiko la Wanafunzi wa Chuo hicho waliokwenda katika
mafunzo kwa vitendo vijijini na kushuhudia namna mabadiliko ya tabia
nchi yalivyoathiri maendeleo ya wananchi”. Alifafanua Prof. Lokina
Tayari
Chuo kina mradi ujulikanao kama Chololo Ecovillage unaofadhiliwa na
Umoja wa Ulaya (EU) Mkoani Dodoma, ambao huwafundisha wanakijiji njia
bora za uzalishaji mali, hivyo kuwafanya baadhi ya Wananchi waliokuwa
wanakosa chakula, kutokana na hali ya Ukame wa Mkoa huo kuanza kupata
mazao ya kutosha na kuongeza pato lao.
Naye
Mkuu wa Chuo hicho cha Mipango ya Maendeleo vijijini- Dodoma, Dkt.
Frank Hawassi, amezitaka Taasisi na Mashirika ya umma na Binafsi
kuunganisha nguvu katika kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia nchi kwa
kuwa kama juhudi hazitachukuliwa athari zake zitampata kila mmoja.
Aidha,
amesema hakuna nchi inayoweza kufanikiwa kukabiliana na tatizo hilo
bila kushirikiana hata kama nchi hiyo imeendelea kwa kiasi kikubwa. Pia
Jamii inapaswa kujua kuwa hata matatizo ya wafugaji, wakulima na wengine
kuhusu ardhi ni matokeo ya athari za Mabadiliko ya Tabia nchi, hivyo
kila mmoja anatakiwa kuwa chachu ya utunzaji wa mazingira, ili
maendeleo yanayopatikana yawe endelevu.
Ameongeza
kuwa Chuo cha Mipango Dodoma kinatoa nafasi kwa wadau kote nchini
kukitumia kikamilifu katika kutatua changamoto za kimazingira kwa kuwa
ipo Idara iliyo na jukumu la kushughulikia suala la Mazingira na
Mabadiliko ya Tabia nchi.
Kwa
upande wake aliyekuwa Balozi wa Umoja wa ulaya nchini Tanzania Tim
Clarke, ambaye ameongoza timu ya washirika wa Maendeleo katika Mkutano
huo ameitaka Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini kujitahidi
kuwahamasisha wananchi kutumia Nishati mbadala ikiwemo Gesi ili
kupunguza kasi ya uharibifu wa misitu kwa kukata miti kwa ajili ya
kupata Mkaa.
Vilevile
ametoa rai kwa Serikali kuwa karibu na jamii na kuwaelimisha kuhusu
kutunza mazingira katika shughuli zao za kila siku za kujipatia kipato
ili kusaidia kulinda mazingira ya asili yatakayochochea kukua kwa uchumi
wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Na Benny Mwaipaja,WFM
Na Benny Mwaipaja,WFM
No comments