Baraza la madiwani Jiji la Arusha ,Robo ya pili lapitisha taarifa mbalimbali za shughuli za maendeleo
Mstahiki Meya wa Jiji Mhe. Kalisti
Lazaro(kushoto) akiteta jambo na Naibu Meya wa Jiji Mhe. Viola Lazaro
Likindikoki wakati wa Kikao cha Baraza.
Wah. Madiwani na wataalam wakifuatilia
kikao cha Baraza
Afisa Utumishi Mkuu wa Jiji. Ndg.
Baltazari Ngowi(Kushoto) akiwa na Kaimu Mwanasheria wa Jiji Fabiola Kisarika
wakati wa Kikao cha Baraza.
Katibu wa Mwenezi wa CCM Arusha Mjini
Gasper Kishumbua(kushoto) akiteta jambo na Katibu wa Chadema Wilaya ya Arusha
Innocent Kisanyage wakati wa Kikao cha Baraz
Nteghenjwa
Hossea, Arusha.
Kikao cha Baraza la Madiwani Jiji la
Arusha kilichoketi kwa robo ya pili kwa mujibu wa kanuni kimepitisha taarifa
mbalimbali za shughuli za maendeleo, kuidhinisha mapendekezo ya Sheria ndogo za
Jiji za mwaka 2006 pamoja kupokea taarifa mbalimbali kutoka kwa Taasisi za
Serikali zinazotoa huduma kwa wananchi wa Jiji la Arusha.
Akifungua Kikao hicho Mstahiki Meya
wa Jiji la Arusha Mhe. Kalisti Lazaro
amewataka wajumbe wa Kikao kuwa makini katika kujadili na hoja mbalimbali
zilizowasilishwa katika Baraza ili kuweza kuleta Tija kwa wananchi wa Jiji na wanaotegemea
kupata maendeleo kupitia vikao.
Naye Mkurugenzi wa Jiji Ndg. Athumani Kihamia alisema kwa
kushirikiana na Menegiment amehakikisha kwamba maazimio yote ya vikao vya awali
yamezingatiwa na miradi imetekelezwa kwa kiwango cha juu huku thamani ya Fedha
ikionekana.
Kutoka katika taasisi zilizoalikwa katika
kikao hicho Mkurugenzi wa AUWSA Eng Ruth
Koya alieza changamoto kubwa inayowakabili wananchi kwa sasa kuwa ni uhaba
wa Maji na kusema kuwa wanategemea kuanza utekelezaji wa mradi mkubwa ambao
utawezesha upatikanaji wa maji Lita Mil 200 wakati mahitaji ni Mil 94 tofauti
na sasa ambapo kiasi kinachohitahjika ni Lita Mil 35 tu ambacho hakitoshelezi
hata nusu ya mahitaji ya wananchi, hivyo kinachohitajika ni ushirikiano wa wadau
na wananchi ili kuweka kufanikisha utekelezaji.
Akiendelea kujibu maswali ya Wah.
Madiwani waliyohoji maji yanayopatikana kuwa na Chumvi Eng. Koya alisema maji ya kisima yanayopatikana Arusha kwa kiasi
kikubwa yana uwekezekano wa kuwa na chumvi kidogo lakini na hayana Flouride tofauti
nay ale ambayo wananchi wanadai ni matamu huwa ni ya yanatokana na Chemchem
ambayo hayapatikani kwa wingi na athari zake ni kuwa na Flouride ambayo
mtumiaji huwezi kuigundua kwa kunywa lakini athari zake huonekana kwenye meno
nk.
Kutoka Tanesco Mhandishi wa Mipango
na Ubunifu Eng.Beatus Rwegoshora
alifafanua tatizo la kukatika umeme mara kwa mara kuwa Tanesco iko katika maboresho
ya huduma kwa wateja nahivyo tatizo hilo litapungua na pia shirika lipo katika
mpango mahususi wa kuwafanya wananchi waweze kupata taarifa zote za msingi
kupitia simu za kiganjani ambapo huduma hiyo itawafanya wananchi kufuatilia na
kupata taarifa kwa wakati na muda wote popote walipo.
Meneja
wa Sumatra Mkoa wa Arusha Bw. Allen
Mwani amesema kwa sasa Mamlaka hiyo ipo
katika upembuzi yakinifu wa mradi wa kuondoa usafiri wa daladala maarufu,
'Vifodi' ambazo hazina viwango katika usafirishaji wa abiria hivyo mpango
uliopo ni wadau kukaa pamoja na kuleta magari makubwa ya usafirishaji wa abiria(City
Bus) katika jiji la Arusha.
Mkurugenzi
wa Fedha na Utawala AICC Ndg. Savo
Mng’ong’o aliwatoa shaka Madiwani waliolalamikia Hospital ya Kituo hicho kutopokea
Kadi za Bima ya Afya (NHIF) ilihali wananchi wanahimizwa kujiunga na mfuko huu
ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za matibabu kwa alifafanua kuwa huduma
hiyo itarejea mwezi Oktoba.
Katika
kikao hiki pia Baraza limepitia na kuidhinisha Sheria ndogo za Halmashauri
ambapo sasa zitawasilishwa Mkoani kisha Tamisemi kwa ajili ya kuidhinisha kisha
kuanza kutumika rasmi. Sheria hizi ni muhimu sana kwa jiji kwa kuwa
zinazotumika sasa ni zile za mwaka 2003.
No comments