MTAZAME MSANII WEMA SEPETU NA WENZAKE WAKIJISALIMISHA POLISI LEO HII, NI BAADA YA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM KUULIPUA MTANDAO WA WAUZA DAWA ZA KULEVYA
Msanii Wema Sepetu akiongozwa na Mmoja wa Makachero wa kituo kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam ili kuripoti kituoni hapo kufuatiwa tuhuma zilizotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda jana wakati alipozungumza na waandishi wa habari katika ofisi zake zilizopo Ilala jijini Dar es salaam, Makonda jana aliutaja mtandao unaojihusisha na uuzaji na matumizi ya madawa ya kulevya jijini Dar es salaam wakiwepo wasanii maarufu na baadhi ya askari wa jeshi la polisi na baadhi ya wamiliki wa klabu za kuuza pombe.
Kamanda wa Kanda Maalum ya Kipolisi Mkoa wa Dar es salaam Kamanda Simon Sirro akiwasili katika kituo kikuu cha polisi kati huku akifuatana na waandishi wa habari mara baada ya kutoka kwenye mkutano wao uliofanyika Oyserbay jijini Dar es salaam.
Msanii Babuu wa Kitaa akiwasili kituo cha Polisi kati jijini Dar es salaam kwa ajili ya mahojiano.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kituo cha Polisi kati ili kujua kinachojiri katika kituo hicho.
Msanii TID akiwasili kwenye kituo cha Polisi Kati jijini Dar es salaam.
No comments