MAKAMU WA RAIS AZINDUA KONGAMANO LA SIKU( 3) LA KISWAHILI ZANZIBAR


  1. Makamu wa Rais Samia Suluhu akizungumza katika uzinduzi wa Kamisheni ya Kiswahili Afrika Mashariki,ikiwa ni Kongamano la Kwanza la Kimataifa lililoshirikisha nchi zaidi ya Sita .Picha na Vero Ignatus Blog.
Waziri mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt.Augustine Mahiga akizungumza na katika kongamano hilo leo Zanzibar.Picha na Vero Ignatus Blog.


Makamu wa Rais Samia Suluhu akizindua mpango mkakati wa Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika ya Mashariki,aliyepo kulia kwake ni Rais mstaafu Tanzania awamu pili Alhaji Ally Hassan Mwinyi,akifuatiwa na Waziri mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt.Augustine Mahiga,wa kwanza kushoto ni waziri wa habari Utamaduni na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe.Picha na Vero Ignatus Blog.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo wakifuatilia kwa makini yale yanayoendelea.Picha na Vero Ignatus Blog.


Rais mstaafu Tanzania awamu pili Alhaji Ally Hassan Mwinyi akiwa na baadhi ya washiriki wa kongamano hilo leo Zanzibar .Picha na Vero Ignatus Blog.


Na,Vero Ignatus Zanzibar

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Hassan Suluhu amezindua rasmi shughuli za Kamisheni ya kiswahili Afrika ya Mashariki likiwa ni Kongamano la kwanza la Kimataifa lililoshirikisha katkribani nchi zaidi ya sita.

Pia amezindua Mpango Mkakati  wa Kamisheni  hiyo unatarajiwa kuanza kutekelezwa na kamisheni hiyo kuanzia sasa.

Makamu wa Rais Samia amesisitiza nchi wanachama zote wataanza kuchangia bajeti kwenye Kamisheni hiyo vilevile kushirikiana katika umoja wa forodha, soko la pamoja, sarafu moja na ushirikiano wa kiasiasa.

Amesisitiza pia suala la mafanikio ya utengamano kamili yanategemea mkabala wa mawasiliano na ushiriki wa raia wote katika maendeleo endelevu ya jumuiya ambapo amesema kuwa lugha ya kiswahili ndiyo inayoweza kufanikisha mamabo  hayo.

Aidha, nchi zilizoshiriki kongamanohilo la kimataifa ni pamoja na Rwanda, Burundi, Sudan Kusini, Uganda, Kenya, DR Congo pamoja na wenyeji Tanzania.

No comments