Mahakama yafuta matokeo ya uchaguzi wa urais Kenya

Mahakama ya Juu nchini Kenya imefutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika mapema mwezi uliopita katika uamuzi kuhusu kesi iliwasilishwa na muungano wa upinzani National Super Alliance.
Muhtasari
Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo akiwa na kura 8,203,290 (54.27%)
Tume ya uchaguzi ilisema Raila Odinga alipata kura 6,762,224 (44.74%)
Upinzani unadai mitambo ya tume ya uchaguzi ilidukuliwa na kuingiliwa kumfaa Rais Kenyatta.
Wakati wa kusikizwa kwa kesi, kulikuwa na mvutano kuhusu kukaguliwa kwa mitambo ya tume ya uchaguzi
Mahakama ya Juu inaweza kuidhinisha au kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi.
Iwapo ushindi wa Rais Kenyatta utaishinishwa, basi ataapishwa Septemba 12
Iwapo uchaguzi utafutiliwa mbali, uchaguzi mwingine utafanyika katika kipindi cha siku 60.
HABARI ZA HIVI PUNDEMaraga: Uchaguzi mpya ufanyike katika kipindi cha siku 60
Jaji Mkuu David Maraga ameagiza: Uuchaguzi wa urais uliofanyika 8 Agosti, 2017, haukuandaliwa kwa mujibu wa katiba na sheria, hivyo matokeo yake ni batili.
"Natangaza hapa kwamba Bw Kenyatta hakuchaguliwa na kutangazwa kwa njia inayofaa.
"Agizo linatolewa, kuagiza Tume ya Uchaguzi kuandaa na kufanyisha uchaguzi mwingine kwa kufuata katiba na sheria katika kipindi cha siku 60."
No comments