Meneja wa TIRA kanda ya Kati bi Stella Rutaguza akitoa ufafanuzi kwa mkuu wa mkoa wa Singida (aliyevaa vitenge) Dkt.Rehema nchimbi, pamoja na mkuu wa mkoa wa Dodoama Mhe.Jordan Rugimbana.Picha na Vero Ignatus Blog.
Mkuu wa mkoa wa Singida (aliyevaa vitenge) Dkt.Rehema nchimbi, akiwa anazungumza na bi Stella Rutaguza kushoto kwake ni mkoa wa Dodoama Mhe.Jordan Rugimbana,wa kwanza kutoka kulia ni Afisa wa bima kutoka TIRA Maneno Adam.Picha na Vero Ignatus Blog.
Na.Vero Ignatus Dodoma
Mamlaka ya Usimamizi wa Bima kanda ya kati (TIRA) Imewaelimisha wananchi juu ya
umuhimu wa wakulima na wafugaji kuhusiana na Bima ya kilimo na mifugo.
Akiongea katika maonesho ya nanenane Kanda ya Kati Dodoma, Meneja wa
Kanda ya Kati Bibi Stella Rutaguza amesema kuwa Mkulima au mfugaji
anapokuwa na bima kwa ajili ya mazao katika shamba lake au mifugo yake
itamuwezesha kupata fidia ya bima kwa kiwango cha hasara anayoipata na
hivyo kuepuka hasara ambayo angeipata kiuchumi kama asingekuwa na bima.
"Unapopata hasara badala ya kulia kilio kisichokuwa na mfariji badala
yake ukiwa na bima utalia huku ukiwa na faraja kuwa mfariji wako bima
yupo na atakufariji kwa kukupatia fidia ya hasara uliyopata, alimalizia
Bibi Stella Rutaguza."
Sambamba na hayo (TIRA) imekuwa ikitoa elimu kwa wananchi pamoja na wamiliki wa vyombo vya moto namna ya kuhakiki na kutambua bima ya vyombo hivyo kama ni halali ili kuepuka kuuziwa bima mbazo ni feki |
No comments