WCS YATOA MSAADAWA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 936 KWA UHIFADHI WA WANYAMAPORI
Katibu
mkuu (mwenye koti nyeusi) akikata utepe wa uzinduzi wa ofisi ya pori la
piti kulia kwake ni kaimu mkurugenzi mkuu wa tawa bw.martin loibooki na
kushoto nimeneja wa pori la rukwa/piti bw.ambrose mungo’ng’o .
Na Mwandishi wetu Songwe
Taasisi
ya Kimataifa ya kijamii ya uhifadhi wa wanyamapori ya World
Concervation Society- WCS imetoa msaada wa zaidi ya shilingi milioni 936
kwa mapori ya akiba ya Lukwati- Piti ambazo zimetumika kujenga jengo la
kisasa la ofisi, ununuzi wa magari matatu ya doria na kuendesha mafunzo
ya askari wa wanyamapori wa mapori hayo yaliyoko mkoani Songwe.
Akiongea
katika halfa ya kukabidhi miradi hiyo kwa serikali ya Tanzania,
Mkurugenzi wa WCS Aaron Nicholaus amesema taaisisi hiyo inajivunia
kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuendeleza shughuli za
uhifadhi wa wanayamapori wakiwemo tembo ambao ni maliasili muhimu
kitaifa na kimataifa ambapo shirika la misaada la watu wa Marekani USAID
nalo ni mdau mkubwa katika ufadhili huo.
katibu mkuu akipokea magari 3 aina ya toyota l/cruiser pickup toka kwa mratibu wa mradi wa cws bw. Aaron nicholaus.
Bwana
Nicholaus alisema msaada huo umetilia mkazo suala la mafuzo ambayo
yatawaongezea askari ujuzi na weledi wa kukabiliana na majangili ambao
wamekuwa wakiua tembo na wanyamapori wengine kwa maslahi yao binafsi na
kusababisha hasara kwa serikali ambayo inawategemea wanyamapori kwa
maendeleo ya jamii na taifa.
“Tunapofikiria
uhifadhi, tuangalie pia masuala ya mapito ya wanyamapori kama tembo
ambayo yamekuwa yakitoweka kutokana na kuongezeka kwa shughuli za
binadamu na hivyo kuathiri uhifadhi maana tembo huhitaji eneo kubwa kwa
malisho” alisme abwana Nicholaus.
Taarifa
ya miradi hiyo iliyotolewa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na
Utalii Meja Jenerali Gaudance Milanzi ilieleza kuwa miradi hiyo ina
thamani kubwa kwa uhifadhi wa mapori hayo yenye ukubwa wa zaidi ya
kilomita za mraba 6,119 ambayo yanapakana na Hifadhi ya taifa ya Ruaha
na pori la akiba la Rungwa.
Katibu mkuu akiongea na baadhi ya kikosi cha askari waliyopata mafunzo ya kukabiliana na ujangili.
Meneja
wa Mapori ya Lukwati Piti Bwana Alphonce Ambroce Mung’ong’o akitoa
ufafanuzo na mchanganuo wa gharama za miradi hiyo alisema jengo la
kisasa la ofisi limegharimu zaidi ya shilingi milioni 227, magari matatu
kwaajili ya doria yana thamni ya dola 255,000 za kimarekani boti na
mfumo wa radio call una thamani ya zaidi ya shilingi milioni 234.
Aidha
Bwana Ambroce alisema wafadhili hao pia wamenunua boti mbili za doria
ambazo zimegharimu zaidi ya shilingi milioni 134 ambazo zitatumika
kuimarisha doria katika ziwa Rukwa ambalo ni miongoni mwa maeneo muhimu
ya mapori hayo ya Lukwati Piti.
Kuhusu
ujangili, Bwana Ambroce alisema katika kipindi cha miaka mitano tangu
mwaka 2013 mpaka sasa zaidi ya tembo 23 wameuwawa kwa ujangili katika
mapori hayo ingawa alisema kwa sasa baada ya mafunzo hayo mapori hayo
yameimarisha doria na amewaonya majangili kuwa sasa serikali imejipanga
kupambana nao kikamilifu.
Bw.martin loibooki (kaimu mkurugenzi mkuu-tawa) akitoa taarifa fupi ya mapori ya akiba rukwa/piti mbele ya katibu mkuu.
“Nawaonya
majangili, sasa tumejipanga kupambana nao na kamwe hatuwezi kuwaacha
waendelee kutamba humu na kumaliza rasilimali zetu kwa manufaa yao, hii
haikubaliki na kamwe hatutawavumilia, tumepata mafunzo na vitendea kazi
lazima tutashinda na kuwaacha wanyamapori watumike kwa shughuli za
kitaifa na kwa maslahi ya watanzania walio wengi” alisisitiza Ambroce.
Akiongea
baada ya kupokea misaada hiyo, Katibu Mkuu wizara ya maliasili na
utalii Meja Jenerali Gaudance Milazi amewashukuru wadau wa uhifadhi
ikiwemo WCS kwa kusaidia juhudi za kuimarisha uhifadhi wa wanyamapori
nchini Tanzania kwani mchango wao umeanza kuzaa matunda.
Meja
Jenerali Gaudance Milanzi alisema Tanzania imejaliwa kuwa na rasilimali
za wanyamapori wengi sana ambao wakitunzwa na kutumika vizuri wana
nafasi kubwa ya kuchangia kwa kiwango kikubwa kuliondoa taifa katika
umasikini uliokithiri na hivyo kuchangia kwa kiwango kikubwa kaika pato
la taifa na maendeleo ya nchi.
Baadhi ya kikosi cha askari kilichohudhuria mafunzo ya kukabiliana na ujangili (rapid response team).
“Kazi
kubwa tuliyonayo ni kuhakikisha rasilimali hizi zinalindwa ipasavyo kwa
manufaa ya vizazi vyote na kamwe asiwepo mtu mwenye uroho wa kutumia
rasilimali hizi kwa manufaa yake binafsi” alisisitiza Meja Jenrali
Gaudance Milanzi.
Alisema
anatambua kabla ya kituo cha Lukwati Piti kuanza mwaka 2013 wavuvi
walikuwa wamesheheni katika fukwe za ziwa Rukwa upande wa pori la akiba
la Likwati, “Hivi sasa kambi hizo za wavuvi zilishaondolewa na fukwe
hizo zimebaki kuwa mazalia mazuri ya mamba ya samaki na malisho ya
wanyamapori hali inayoleta matumaini ya kuimarika kwa uhifadhi wa
wanyamapori” alisema Meja jenerali Milanzi.
Meja
jenerali Gudance Milanzi alitumia fursa hiyo kuwaonya baadhi ya wananchi
wakorofi wajiepushe kufanya za binadamu ikiwemo uanzishaji wa makazi,
kilimo, uvuvi, uchimbaji wa madini na uingizaji wa mifugo kwenye maeneo
yaliyohifadhiwa kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria za uhifadhi.
“Sasa
maeneo mengi ya hifadhi yanakumbwa na changamoto za ongezeko la shughuli
za binadamu ikiwemo uingizaji wa mifug itambulike kwamba maeneo ya
hifadi yametengwa kisheria kwa shughuli za uhifadhi na wanaofanya mchezo
huo waache mara moja na sheria itaendelea kuchukua mkono wake kwa
wafugaji na mifugo inayokamatwa” alionya.
Meja
jenerali Gudance Milanzi alisema serikali itaendelea kuchukua hatua
mbalimbali kuhakikisha masuala ya ujangili yanadhibitiwa ikiwa ni kuweka
mazingira mazuri ya utendaji kazi kwa watumishi wake, kununua vitendea
kazi ikiwemo magari ya doria.
Alisema
juhudi hizo ni pamoja na kugeuza mfumo wa kiutendaji kutoka ule kiraia
na kwenda mfumo wa jeshi usu na akaipongeza Mamlaka ya wanyamapori TAWA
kwa kutoa kipaumbele katika mafunzo kuelekea mfumo wa jeshi usu ambapo
katika kipindi cha mwaka mmoja TAWA imetoa mafunzo kwa watumishi 236.
Mapema
katika taarifa yake kwenye hafla ya kupokea miradi hiyo kutoka WCS
iliyofanyika kwenye ofisi za pori hilo zilizoko Lupatingatinga wilayani
Songwe, kaimu Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya Wanyamapori TAWA Martini
Loibooki alisema ufadhi wa WCS katika mapori hayo ni matokeo ya
ushirikiano unaoendelea kati ya TAWA na wadau wa uhifadhi.
Bwana
Loibooki alisema WCS imekuwa mfadhili wa kwanza kuingia kufadhili mapori
ya Lukwati Piti ambayo hko nyuma yalikuwa na changamoto nyingi ikiwemo
ujangili na uwindaji haramu lakini kutokana na ufadhili huo sasa
uhifadhi umeanza kuimarika.
Alisema
amepokea changamoto za kituo cha Lukwati Piti lakini Mamlaka imeweka
mipango ya muda mfupi na muda mrefu kuhakikisha changamoto hizo
zinaendelea kupungua kadri upatikanaji wa fedha na kwamba mazingira ya
kazi yameanza kuwa bora na vitendea kazi vimeongezeka na kuwa bora
kuliko miaka ya nyuma.
Alieleza
kuwa mapori ya Lukwati Piti yana umuhimu mkubwa na yamekuwa chanco
muhimu cha mapato ya serikali kutokana na uwindaji wa kitalii ambapo
katika kipindi cha miaka mitano iliyopita mapori hayo yameliingizia
taifa mapato ya zaidi ya shilingi bilioni mbili na milioni mia tisa.
Bwana
Loibooki alisema fedha hizo zinazotokana na uwindaji wa kitalii ni
nyingi na zimeisaidia serikali kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo
kwenye mikoa mbalimbali nchini ikiwemo afya , elimu na ujenzi wa miradi
ya kijamii.
Kaimu
mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya wanyamapori tanzania tawa, martin loibooki
amesema tawa inatambua wajibu wake na malengo ya kuanzishwa kwa mamlaka
hiyo ya kusaidia kuchochea maendeleo ya jamii na kukuza uchumi wa nchi
kupitia sekta ya wanyamapori na ameishukuru wcs kwa kuwa mfadhili wa
kwanza kufadhili shughuli za uhifadhi katika mapori ya lukwati- piti.
No comments