Waziri Masauni:Ole wao Polisi wasiotimiza wajibu wao kikamilifu.

Na.Vero Ignatus,Dodoma.
Waziri wa mambo ya ndani Hamad Masauni amewaonya askari Polisi wasiotimiza wajibu wao kikamilifu amesema kuwa serikali haitalifumbia macho jambo hilo
Ameyasema hayo mjini Dodoma katika siku ya mabalozi wa usalama barabarani (RSA) yaliyofanyika katika uwanja wa Mashujaa ambapo anasema kuwa wapo baadhi ya askari wasiofanya wajibu wao serikali itawashughulikia
"Nafahamu kuwa askari wanafanya kazi katika mazingira magumu na yenye ushawishi mkubwa hawa lazima wapongezwe,lakini wale ambao wanakwenda kinyume na maadili ya kazi yao ole wao".alisema.
Aidha amemuagiza Kamanda wa usalama barabarani Mohamed Mpinga kuwathibiti vijana eneo la Kigamboni ambao wanaokiuka na kuvunja sheria za usalama barabarani
Amepiga marufuku madereva wa bodaboda kuwapakiza watoto wa miaka 3 bila kuwa na uangalizi wa mzazi au mtu mzima yeyote atakayekiuka sheria ya usalama barabarani achukuliwe hatua ,kwani waendesha pikipiki wanaongoza kwa kuvunja sheria za barabarani.
"Wapo baadhi ya madereva bodaboda wanaopakiana watatu au wanne huku wakiendesha kwa kasi naagiza fuatilieni hilo na mlidhibiti kwani wanaongoza kuvunja sheria, ni marufuku kuwapakiza watoto wa miaka 3,ukimpakiza awe chini ya uangalizi wa mtu mzima."alisema.
No comments