RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA AKABIDHI NYUMBA 50 ZA WATUMISHI WA AFYA KATIKA MIKOA YA SIMIYU, KAGERA NA GEITA
Rais
Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa akimkabidhi Hati za Umiliki wa
nyumba 50 za Watumishi wa Afya kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika uwanja wa michezo wa Mazaina
Chato mkoani Geita.
Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa akizungumza na wananchi wa
Mikoa ya Geita, Simiyu na Kagera katika uwanja wa Mazaina Chato mkoani
Geita kabla ya kukabidhi Hati za umiliki wa nyumba 50 za watumishi wa
sekta ya Afya zilizojengwa na Taasisi ya (Mkapa Foundation) katika mikoa
hiyo mitatu.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na wananchi wa Mikoa ya Geita, Simiyu na Kagera katika uwanja wa
Mazaina Chato mkoani Geita baada ya Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu
Benjamin Mkapa kukabidhi nyumba 50 kwa wizara ya Afya.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru
Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa mara baada ya kukabidhi
nyumba hizo 50 zitakazotumika katika Sekta ya Afya katika mikoa ya
Kagera, Simiyu na Geita.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia
jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa wakati Mbunge wa
Chato ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard
Kalemani alipokuwa akihutubia wananchi wa Chato mkoani Geita.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na
Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa mara baada ya kumaliza
ziara yake Chato mkoani Geita ambapo alikabidhi nyumba 50 zitakazotumika
katika sekta ya afya katika mikoa ya Geita, Simiyu na Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mama Anna Mkapa.
Rais
Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa akiangalia hotuba yake kabla ya
kuhutubia wananchi mbalimbali katika uwanja wa michezo wa Mazaina Chato
mkoani Geita.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiwasalimia wananchi wakati akiwasili katika uwanja wa Mazaina Chato
mkoani Geita.
Kikundi cha ngoma za asili cha Chato kikitumbuiza katika uwanja wa Mazaina Chato mkoani Geita.
Balozi
wa Japan hapa nchini Masaharu Yoshida akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya
Chato Shaaban Ntarambe hati ya kituo cha kukamua Mafuta ya Alizeti
(Double Refine) kilichojengwa Chato mkoani Geita kwa Msaada wa Serikali
ya Japan.
PICHA NA IKULU





















No comments