RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA WATUMISHI WA ILIYOKUWA BRN NA JOPO LA WATAALAMU WA NISHATI NA MIUNDOMBINU YA MABWAWA YA KUZALISHA UMEME
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na
watumishi wa iliyokuwa Presidential Delivery Bureau (PDB) waliokuwa wakisimamia utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now - BRN alipokutana nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2017
Brn
3: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli
akipata picha ya pamoja na na watumishi wa iliyokuwa Presidential
Delivery Bureau (PDB) waliokuwa wakisimamia utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now - BRNalipokutana nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2017
Picha ya pamoja
Brn4:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli
akiagana na na watumishi wa iliyokuwa Presidential Delivery Bureau
(PDB)waliokuwa wakisimamia utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now - BRN baada ya kukutana nao Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na jopo la wataalam
wa masuala ya umeme na ujenzi wa miundombinu ya mabwawa ya maji kwa
ajili ya kuzalisha umeme na kujadiliana nao kuhusu utekelezaji wa mradi
mkubwa wa uzalishaji wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge Power Project) ambao una uwezo wa kuzalisha Megawatts 2,100 za umeme Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2017. PICHA NA IKULU
Wafanyakazi
hawa ndio walikuwa wakisimamia utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now - BRN).
Mhe.
Rais Magufuli amekutana na wafanyakazi hao Ikulu Jijini Dar es Salaam ambapo
amewashukuru kwa kazi nzuri waliyoifanya wakiwa PDB na amewataka kuendelea
kulitumikia Taifa kwa juhudi na maarifa wakiwa katika ofisi nyingine
walizopangiwa.
“Natambua
kuwa nyie ni wafanyakazi wazuri wenye ujuzi na maarifa muhimu kwa ajili ya
Taifa letu. Mmetoa mchango mkubwa mlipokuwa PDB nategemea mtaendelea hivyo na
hata zaidi katika ofisi mbalimbali mlizopangiwa, mkachape kazi kwa kutanguliza maslahi
ya Watanzania” amesema Mhe. Rais
Magufuli.
Mkutano
huo umehudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
Mhe. Angellah Kairuki na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Laurian Ndumbaro.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amekutana na
timu ya wataalam wa masuala ya umeme na ujenzi wa miundombinu ya mabwawa ya
maji kwa ajili ya kuzalisha umeme na kujadiliana nao kuhusu utekelezaji wa
mradi mkubwa wa uzalishaji wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge Power Project) ambao una uwezo wa kuzalisha Megawatts 2,100 za
umeme.
Mhe. Rais Magufuli amekutana na
wataalamu hao ikiwa ni utekelezaji wa nia yake ya kuhakikisha mradi huo unaanza
kujengwa haraka iwezekanavyo na kuzalisha umeme mwingi utakaosaidia kuharakisha
maendeleo hapa nchini, hususani ujenzi wa viwanda.
“Kesho Waziri Mkuu wa Ethiopia
Mhe. Hailemariam Desalegn anawatuma wataalamu wake waliojenga mradi mkubwa wa
bwawa la maji la kuzalisha umeme kule Ethiopia, wakiwa hapa mtakutana nao na
mtabadilishana uzoefu, nataka na sisi tusichelewe, tuzalishe umeme utusaidie
kwenye ujenzi wa viwanda” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,
IKULU
Dar es Salaam
27 Juni, 2017






No comments