FAO YAAHIDI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI ILI KUHAKIKISHA WAKULIMA WANAZALISHA CHAKULA CHA KUTOSHA
Baadhi ya wakulima walioshiriki katika maonyesho hayo yaliyofanyika kwa siku mbili katika kituo cha utafiti cha Selian.Picha na Vero Ignatus Blog.
Baadhi ya wakulima wakipate elimu kwenye shamba darasa katika maonyesho hayo yaliyofanyika katika kituo cha utafiti cha Seliani.Picha na Vero Ignatus Blog.
Baadhi ya wadau wa zana za kilimo walioshiriki maonyesho hayo kutoka kampuni ya Wade Rain.Picha na Vero Ignatus Blog.
Afisa Maendeleo Biashara kutoka Asasi isiyo ya kiserikali (PASS) Ayubu Mbezi (aliyevaa tisheti ya njano pichani)akitoa elimu kwa mkulima namna ambayo mkulima anaweza kuunganishwa na Taasisi hiyo kupata mkopo benki na kuwaonngezea dhamana aliyepo kulia kwake ni Peter Msechu mfanyakazi katika Taasisi hiyo.PASS inajishughulisha kusaidia sekta ya kilimo,iliyoanzishwa mwaka 2000 ili kuchbochea uwezeshaji na kukuza kilimo cha biashara na sekta zinazohusika.Picha na Vero Ignatus Blog.
Mkufunzi Happy Martin kutoka Taasisi isiyo ya kiserikalia (ECHO)dawa i akitoa elimu kwa wakulima namna ya kuhifadhi mbegu katika mazingizra maziri bila kuziweka dawa Mbegu bora zinatzoweza kama mbolea,mbegu.Picha na Vero Ignatus Blog.
Na.Vero Ignatus .Arusha
SHIRIKA la chakula Ulimwenguni, FAO, limeahidi kuendelea kushirikiana
na serikali katika kuhakikisha wakulima wanazalisha chakula cha kutosheleza na hivyo kuondoa tatizo la uhaba wa chakula kwa baadhi ya maeneo hapa nchini.
Mwakilishi wa FAO ,Fred Caferody,ameyasema hayo
alipokuwa akitoa salamu kwenye siku ya wakulima wa mazao mchanganyiko ya
chakula na biashara kutoka mikoa mbalimbali nchini yaliyofanyika kwenye viwanja
wa Taasisi ya utafiti wa mazao, Seliani jijini Arusha.
Kwa upande wake Muwakilishi wa Baraza la nafaka la Afrika mashariki, (EAGC),hapa nchini Ikunda Materu alimesema litaendelea kushirikiana na vituo vya utafiti wa mazao ya kilimo kwa nchi za afrika mashariki katika kutafuta masoko ya nje wakulima nchini.
Amesema FAO, imekuwepo hapa nchini kwa miaka 40 imekuwa
ikiandaa sera na programu mbalimbali za kilimo na chakula ili kuwezesha wakulima
kuzalisha chakula kinachotosheleza mahitaji kwa kushirikiana na serikali na
swala la kilimo na chakula ni sehemu ya jukumu lake kuhakikisha hakuna
upungufu wa chakula nchini.
Mkurugenzi wa fedha wa shirika hilo Drollah Ssebagala,
amesema baraza la nafaka litakuwa
likiwapatia wakulima taarifa za masoko
kwenye nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia DRC congo, Malawi
na Zambia Sudani na Ethiopia
Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa utafiti wa mazao nchini
kutoka wizara ya Kilimo na Mifugo, Dakta Jackson Nkuba, amesema upo ugonjwa wa
Manjano unaoshambulia mahindi na hilo ni
tatizo kubwa hivi sasa serikali kupitia wizara ya kilimo imeweka nguvu kubwa
ili kuudhibiti ugonjwa huo.
Amesema kuwa ugonjwa
huo ni tatizo kwa kuwa unashambulia mahindi yakiwa shambani na kunyauka hivyo
mkulima anapata hasara .
Amesema kuwa hayo ni maonyesho ya nne ya mnyororo wa mazao
ya kilimo kufanyika nchini ni maonyesho muhimu sana na yatapanuliwa katika
kanda zingine nchini lengo ni kuwezesha wakulima kupata teknolojia ya kilimo
cha biashara kutoka kilimo cha kujikimu .
Hivyo akayataka makampuni ya uzalishaji wa mbegu bora kutoka kwenye taasisi za
utafiti wa mbegu ambayo yataongezeka ili kuwafikia wakulima ili kuwafikia
wakulima waweze kuzalisha mazao bora na kulima kilimo cha kibiashara.
Akifungua maonyesho hayo Katibu tawala wa mkoa wa Arusha,
Richard Kwitega, amesema mpango wan chi katika kilimo ni kuendelea
kushirikiana na baraza la Nafaka la nchi
za afrika mashariki,shirika la kilimo na chakula ulimwengini, FAO na wadau wengine
Amewataka watafiti wa mbegu kuhakikisha matokeo ya uutafiti
wanazofanya yanawafikia wakulima ili kuweza klkuleta tija vinginecvyo
yasiopowafikia walengwa hayawezi kuleta tija kwenye kilimo.
Amezitaka taasisi zingine binafsi kuongeza ushirikiano na
serikali ili kuharakisha maendeleo na upatikanaji wa mbegu bora za mazao aina
mbalimbali za mazao.
Amesema uzalishaji mdogo wa mazao unachangiwa na kilimo kisichozingatia utaalamu ,ukosefu wa
masoko mazao kushambiliwa na magonjwa ucheleweshwaji wa pembejeo kutokuwepo kwa vikundi vya wakulima miundo
mbinu hafifu ya kuhifadhia mazao na
kuendelea na kilimo cha kizamani.
Hivyo akatoa wito kwa wataalamu wa kilimo kuanzisha mashamba
darasa kila eneo ili wakulima waweze kupata elimu na kubadilisha mbinu za
kilimo kutoka cha kujikimu na kuwa cha kibiashara.
Akawataka viongozi wa vijiji kihakikisha kila kaya inatenga
hekari moja yitakayotokana na kilimo cha mazao yanayotokana na mbegu bora
zilizofanyiwa utafiti na hivyo kuharakisha mabadiliko .

No comments