MKUU WA MKOA WA MANYARA AZINDUA KAMPENI YAUPANDAJI MITI MERERANI


Mkuu wa mkoa manyara mh Joel Bendera akipanda mti katika shele ya sekondari Mirerani B.W.Mkapa

Akizungumza na wananchi katika  ziara yake ya siku moja katika mji mdogo wa mirerani na mh joel benderaa amesema lazima nchi ijifunze kwa kupitia manyara kwamba mazingira ni muhimu hivyo amezindua kampeni ya kupanda miti katika shule ya sekondari ya mireran b.w mkapa yenye ushindani wakutuza mti
Manyara,Mererani

Mkuu wa mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera  amezindua kampeni ya upandaji miti katika mji wa Mererani,wilaya ya Simanjiro huku akitoa wito wananchi mkoa wa Manyara kuzitumia mvua zinazonyesha kupanda miti ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.


Akizungumza katika uzinduzi huo juzi, ambao umeanzishwa na kampuni ya Tanzanite One, katika shule ya Sekondari, Benjamin Mkapa,Dk Bendera alisema,mji huo ambao kwa kawaida hauna mvua za kutosha unapaswa kutumia mvua zinazoendelea kupanda miti.


“kila kaya lazima ipande miti sasa,ili kuondoa hili jangwa na kutokana na mvua hizi tunauhakika miti mingi inakuwa na kubadilisha kabisa mazingira ya Mererani”alisema


Akizungumzia mradi huo, Mkurugenzi wa Tanzanite One, Hussein Gonga alisema,kampuni hiyo, imejipanga kuondoa tatizo la ukame Mererani, kwa kuanzisha kampeni ya kupanda miti 1000 awamu ya kwanza.


Gonga alisema  kampuni hiyo, imetenga kiasi cha sh 4milioni, kwa wanafunzi wa shule ya Benjamin Mkapa ambao watafanikisha mradi huo, kwa njia ya kushindana madarasa manne, kidato cha kwanza hadi cha nne.


“darasa ambalo miti yake, itakuwa vizuri litapata zawadi y ash 2.5 milioni, washindi wa pili 1 milioni na washindi wa tatu 500,000 lengo ni kuhakikisha miti yote 1000 inakuwa”alisema


Alisema dunia hivi sasa inakabiliwa na tatizo kubwa la mabadiliko ya tabia nchi,maeneo mengi kuna ukame,wanyama na binaadamu hawana mvua na maji hivyo, njia pekee ya kujikomboa ni kupanda miti.


Kwa upande wake,Mkurugenzi mwenza wa kampuni hiyo, Faisal Shabhai alisema,baada ya kampeni hiyo, kufanikiwa katika shule ya Benjamin Mkapa,watahakikisha inahamia katika shule nyingine za Mererani na katika vikundi vya utunzwaji wa mazingira.


Mwalimu Mkuu wa shule ya Benjamin Mkapa, Emmanuel Kato,alisema mradi huo utasaidia kupunguza tatizo la ukame Mererani naa pia kuboresha mazingira ya shule na Mererani kwa ujumla.


“tunaishukuru kampuni ya Tanzanite One kwa kuleta hapa shuleni kwetu mradi huu na pia wameahidi kutujengea uzio wa kuzunguka shule na kuboresha  kisima kirefu cha maji ambacho walituchimbia illi tupate maji ya kutosha”alisema


Mwanafunzi wa shule hiyo, Aisha Abdi alisema, wamejipanga kila darasa kuhakikisha wanashinda zawadi  kwa kuitunza vyema miti waliyopanda ambayo pia itasaidia kuboresha hali ya hewa katika shule hiyo.

No comments