*RC Gambo akutana na Kamisha Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji*
ARUSHA
Mkuu
wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo leo amekutana na Kamishna Jenerali
wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Ndg. Thobias Andengenye ofisini kwake.
Katika
mazungumzo yao wamekubaliana kuendelea kushirikiana katika kufanya kazi
na pia jeshi la zimamoto na uokoaji wameomba ushirikiano toka kwa mkuu
wa mkoa ili kuweza kuliunganisha jeshi hilo na mamlaka za serikali za
mitaa ili liweze kufanya shughuli zake kwa ufanisi kwani mnufaika mkubwa
wa huduma zao ni mamlaka hizo husika.
Mhe. Mrisho Gambo
ametoa rai kwa Jeshi hilo kuacha kufanya kazi kwa mazoea badala ya
kusubiri matukio ya ajali za moto kutokea wanapaswa kutoa elimu kwa
wananchi namna ya kuyazuia matukio hayo na kwa kufanya hivyo watapunguza
sana kazi yao kwani majanga ya moto yatakua historia.
Pia
wamekubaliana kuhakikisha ramani za majengo na michoro ya mpango
kabambe (master plan) kwa jiji la Arusha zinapitiwa, lengo ni kuona
mapungufu ya kiusalama dhidi ya majanga ya moto na kuona namna ya
kuzitatua mapema.
Mkoa wa Arusha hasa kwa jiji la Arusha ni miongoni mwa maeneo ambayo kuna changamoto kubwa sana hasa panapotokea majanga ya moto kwani miundo mbinu na vituo vya zimamoto havitoshelezi mahitaji.
No comments