JIJI LA ARUSHA LAADHIMISHA JUMA LA ELIMU, SHULE YA LUCKY VICENT YANG'ARA KIELIMU
1 Katibu
Tawala wa Wilaya ya Arusha Ndg. David Mwakiposa akizungumza wakati wa
maadhimisho ya Juma la Elimu katika Jiji la Arusha.
2 Kaimu
Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi Bi. Eunice Tondi akisoma taarifa katika
maadimisho ya juma la Elimu yaliyoadhimishwa katika viwanja vya Arusha School
jijini hapa.
3 Mgeni
rasmi ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha Ndg. David Mwakiposa(kwanza
kushoto) akitembelea maonyesho wakati wa Juma la Elimu lililofanyika katika
viwanja wa Arusha School.
4 Wanafunzi
wa shule mbalimbali pamoja na walimu wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa
sherehe za Juma la Elimu
Katibu Tawala wa Wilaya Ndg. David Mwakiposa(kushoto) akikabidhi cheti cha Ushindi kwa kuwa nafasi ya kwanza kiwilaya kwa Mwl. Mkuu wa Shule ya Lucky Vicent Bw. Innocent Mushi.
Wanafunzi
wa darasa la nne wakifurahi maadhimisho ya Juma la Elimukatika viwanja vya
Arusha School.
ARUSHA.
Shule ya msingi Lucky Vicent yaibuka na mshindi wa
Jumla Kitaaluma kwa kushika nafasi ya kwanza Kimkoa katika maadimisho ya Juma
la Elimu yaliyoadhimishwa katika viwanja vya Arusha School jijini hapa.
Shule hiyo iliyopata na msiba wa wanafunzi 32, walimu 2
pamoja na dereva kutokana na ajali ya
Coastal hivi karibuni imefanya vizur katika mitihani ya darasa la saba
iliyofanyika mwaka 2016 katika ngazi ya Mkoa na Wilaya hivyo kujinyakulia Kombe
pamoja na Cheti.
Akipoka zawadi hizo za Ushindi Mwel Mkuu wa Shule hiyo Bw.
Innocent Mushi alisema wanafarijika kupata zawadi hizo ingawa bado simanzi na
majonzi yametanda shuleni kwa wanafunzi pamoja na uongozi wa shule hiyo.
“Tunamshkuru Mungu kwa Shule yetu kufanya vizuri na hizi ni jitihada za walimu kufanya kazi kwa
bidii pamoja na wafunzi kuzingatia yale
wanayofundishwa na walimu wao hakika zawadi hizi zimetupata faraja katika
kipindi hiki kigumu tunachopitia.” Alisema Mwl. Mushi.
Katibu Tawala wa Jiji la Arusha Ndg. David Mwakiposa ambaye ndiye
mgeni rasmi katika maadhimisho hayo
amepongeza shule zote zilizofanya vizuri Kitaaluma kwa mwaka
uliopita ikiwa ni pamoja na Walimu na
Wanafunzi na pia alitembelea miradi ya kiubunifu inayoendeleza sanaa za
wanafunzi ikiwa ni pamoja na kuwawezesha kupata ajira hapo baadae.
Mwakiposa alisema “Taifa lolote haliwezi kuendelea pasipo
wananchi wake kuelimika hivyo nichukue fursa hii kuweka msisitizo kwa walimu na
viongozi mbalimbali katika sekta ya
elimu kufundisha wanafunzi kwa weledi na kutoa elimu bora ili malengo mbalimbali ya
kitaaluma yaweze kufikiwa”
Pia aliongeza kwa kusema kuwa amefurahishwa na kuhamasishwa
sana katika maonyesho yaliyofanywa na wanafunzi hasa maonyesho ya mafunzo ya
kitaaluma, kisayansi na ufundi stadi na
kusisitiza kuwa endapo watashirikisha jamii taaluma walizofundishwa na walimu wao na wakiwezeshwa na wadau wa
elimu basi Tanzania yetu itapiga hatua kubwa hasa katika suala zima la uchumi
wa viwanda.
Miongoni mwa maonyesho yaliyoweza kuonyeshwa na wanafunzi wa kawaida na wenye ulemavu ikiwemo viziwi, matatizo ya
akili na wasioona ni pamoja na utaalamu wa kusindika maparachichi na
kutengeneza mafuta yanayoweza kutumika kama kilainishi katika
karakana za vyuma vyenye kutu na dawa ya
ngozi, ujuzi wa kutengeneza dawa ya kung’arishia viatu pamoja na ushonaji wa nguo na vitambaa vya kupambia
majumbani.
Pia wanafunzi walionyesha namna ya kuzalisha umeme kwa kutumia nyaya,
utengenezaji wa mapambo kwa kutumia shanga zinazotokana na makaratasi na watoto
wenye ulemavu wa kusikia wanavyoweza kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
(TEHAMA)katika kujifunza mambo mbali
mbali.
Maadhimisho ya Juma la Elimu hufanyika kila mwaka lengo ikiwa
ni kutathimini ubora wa Elimu, kuwatambua waliofanya vizuri kitaaluma na
kuonyesha kwa vitendo ubunifu wa wanafunzi na sanaa inavyokua katika sekta ya
Elimu.
No comments