UFUNGUZI WA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA SARPCCO WAFANYIKA JIJINI ARUSHA LEO.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Mhe.Hamad Masauni akizungumza na
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu wakati anawasili katika ukumbi
wa mikutano wa AICC kwa ajili ya ufunguzi wa Mkutano mkuu wa mwaka wa Shirikisho
la Wakuu wa Polisi kutoka nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO). Kulia ni Mkuu wa
INTERPOL kanda ya Kusini Mubita Nawa.( Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi)
Katibu
Mtendaji wa SADC, Dk.Stegnomena Tax akizungumza na Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini IGP Ernest Mangu kabla ya ufunguzi wa Mkutano mkuu wa mwaka wa
Shirikisho la Wakuu wa Polisi kutoka nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO)
unaofanyika mkoani Arusha. IGP Mangu ndiye Mwenyekiti wa shirikisho hilo kwa
kipindi hiki. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi)
Baadhi
ya Wakuu wa majeshi ya Polisi kutoka nchi za kusini mwa Afrika SADC wakitoa
heshima wakati wimbo wa taifa unapigwa wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano
mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi kutoka nchi za kusini mwa Afrika
(SARPCCO) uliofanyika Mkoani Arusha. IGP wa Tanzania, Ernest Mangu ndiye
Mwenyekiti wa shirikisho hilo kwa kipindi hiki. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la
Polisi)
Katibu
Mtendaji wa SADC, Dk.Stegnomena Taxi, akitoa hotuba wakati wa hafla ya ufunguzi
wa Mkutano mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi kutoka nchi za kusini
mwa Afrika (SARPCCO) Mkutano huo ulifunguliwa na Naibu Waziri wa Wizara ya
Mambo ya ndani ya nchi, Mhe.Hamad Masauni Mkoani Arusha. IGP wa Tanzania Mangu
ndiye Mwenyekiti wa shirikisho hilo kwa kipindi hiki. Picha na Hassan
Mndeme-Jeshi la Polisi)
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Mhe.Hamad Masauni akiwa katika
picha ya pamoja na Wakuu wa Polisi kutoka nchi za kusini mwa afrika (SARPCCO)
baada ya ufunguzi wa Mkutano mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi
kutoka nchi za kusini mwa Afrika unaofanyika Mkoani Arusha. Picha na Hassan
Mndeme-Jeshi la Polisi.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest
Mangu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) akiwa ameambatana na
Mkuu wa Jeshi la Polisi la Angola, Paulo de Almeida (kushoto) na Mkuu wa jeshi
la Polisi la Msumbiji, Paulo Chachine (kulia) wakati wa Mkutano mkuu wa mwaka
wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi kutoka nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO)
uliofanyika Mkoani Arusha.(Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.
Na.Vero Ignatus ,Arusha.
Mkuu Wa jeshi la Polisi Nchini Tanzania IGP Ernest Mangu
amekuwa umoja unaounda nchi zilizopo kusini mwa Africa (SARPCO )zitahakikisaha kuwa zinaimarisha swala la ulinzi na usalama ili kuweza
kuleta maendeleo katika nchi 15 zinazounda umoja huo.
Ameyasema hayo katika ufunguzi
wa Mkutano mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi kutoka nchi za kusini
mwa Afrika (SARPCCO)
ulioshirikisha nchi 15 zilizounda umoja,ambao umefanyika katika kituo
cha kimataifa cha mikutano (AICC) uliopo mkoa Wa Arusha.
IGP Mangu amesema kuwa lengo la Mkutano huo nikuendeleza
mashirikiano kati ya nchi hizo ,ualifi unaovuka mipaka ,udhibiti Wa
madawa za kulevya,ambazo zimekuwa ni changamoto kubwa Pamoja na
uharamia.
Katubu mtendaji wa SADC Dk.Stegnomena Tax amesema kuwa amezungumzia suala LA kuweka mikakati na Sera za kuwa pamoja na kujipanga ili kuweza kutokomeza biashara haramu ya kusafirisha binadamu haswa mama na mtoto.
"Hali yeyote ya kupambana na uhalifu lazima ushirikiane na nchi za jirani peke yako huwezi kutokomeza sawa za kulevya,biashara haramu ya binadamu,usafishaji Wa fedha,kuhakikisha mazingiravyetu yapo salama,na kukomesha uharamia"alisema Katibu mtendaji Wa SADC.
Naibu waziri Wa Mambo ya ndani Injinia Ahamad Masauni amezitaka nchi hizo za (SARPCCO)washirikiane kimalengo,kimkakati,na kuhakikisha majeshi ya nchi hizo yanakuwa ya kisasa,wafanye mafunzo kwa pamoja kwa kubadilishana taarifa.
" Tatizo la biashara haramu ya kusafirisha Binadamu siyo kwa SADC peke yake ,bali ni tatizo linaloikumba dunia nzima kama takwimu zinavyoonyesha"alisema Masauni.
No comments